CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA) CHAJIPANGA VYEMA KUDAHILI WANAFUNZI WAPYA
CHUO KIKUU CHA TAIFA ZANZIBAR (SUZA) CHAJIPANGA VYEMA KUDAHILI WANAFUNZI WAPYA.
Na Thadei Praygod
Dar es salaam.
Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA)kimesema kimejipanga vyema katika kudahili wanafunzi wapya katika mwaka wa masomo 2021/2022 na kuhakikisha kinaendelea kutoa elimu bora.
Hata hivyo chuo hicho kimesema kitaendelea kutoa elimu zenye ubora na kiwango cha hali ya juu ili kuwapeleka katika soko la ajira wahitimu waliokidhi kiwango cha soko hilo.
Aidha kimewataka wanafunzi kutembelea banda lao ili kupata msaada, maelekezo pamoja na ushauri nasaha kuhusu kozi mbalimbali zinazotolewa katika chuo hicho ambazo zitawasaidia katika masomo yao ya elimu ya juu.
Afisa udahili wa chuo hicho, Ali Shauri Jecha ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya 16 ya vyuo vya elimu ya juu Sayansi na Teknolojia yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
Ameongeza kuwa,wapo katika maonyesho hayo kwa ajili ya kutoa msaada wa kujiendeleza kielimu pamoja na kuonyesha miradi inayofanyika chuoni hapo ambapo jumla ya kozi 62 zinatolewa katika ngazi zote kwa kada mbalimbali ikiwemo afya, ualimu pamoja na Utalii.
Aidha, chuo hicho kinatarajia kudahili zaidi ya wanafunzi 3200 katika kozi mbalimbali katika mwaka wa masomo 2021/22 katika ngazi ya cheti, stashaha, shahada pamoja na masters.
Chuo hicho, kinatoa kozi mbalimbali ikiwemo Kilimo na ufugaji, Utalii,Ugavi na Ununuzi,Sayansi ya kompututa, Uandishi wa habari, Afya ikiwemo ukunga na uuguzi, Sayansi ya Afya ya mazingira pamoja na mafunzo ya lugha ya Kiswahili ambayo inahusisha watu kutoka mataifa mbalimbali.
Hata hivyo kozi zinzotolewa na chuo hicho kwa ngazi ya uzamili[masters] na uzamivu[PhD] ni pamoja na .
1. SHAHADA YA UZAMILI YA SAYANSI YA KEMIA.
2. SHAHADA YA UZAMILI YA SAYANSI YA MAZINGIRA.
3. SHAHADA YA UZAMILI YA SAYANSI YA MABADILIKO YA TABIA YA NCHI
NA UDHIBITI WA RASILIMALI.
4. SHAHADA YA UZAMILI YA SAYANSI YA TEKNOLOJIA HABARI.
5. SHAHADA YA UZAMILI YA ELIMU YA VIJANA, JINSIA NA MAENDELEO.
6. SHAHADA YA UZAMILI YA ELIMU YA KUFUNDISHA KISWAHILI KWA
WAZUNGUMZAJI WA LUGHA NYENGINE.
7. SHAHADA YA UZAMILI YA ELIMU YA LUGHA NA MAENDELEO YA ELIMU.
8. SHAHADA YA UZAMIVU YA KISWAHILI.
9. SHAHADA YA UZAMILI SANAA YA KISWAHILI
na unaweza kuwasiliana nao kupitia tovuti yao ya www.suza.ac.tz au
https://suza.osim.cloud
au kwa simu namba +255 777 453 330; +255 777 86 8116 NA +255
773 124 938
Comments