MGOMBEA UDIWANI KATA YA MBAGALA KUU AWAAHIDI NEEMA WAKAZI MTAA WA KIZUIANI.

 





Dar es salaam

Mgombea udiwani kata ya Mbagala kuu wilayani Temeke,Dar es salaam MAANYA JUMA MAANYA amewaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua ili awatatulie kero zao ikiwemo kero ya upatikanaji wa maji safi na salama inayowakabili. 

Mgombea huyo ameyasema hayo atika mtaa wa kizuiani wakati akiendelea na kampeni zake za uchaguzi mdogo katika kata ya Mbagala kuu ambapo amesema endapo wananchi watampatia ridhaa ya kuwaongoza kama diwani atahakikisha pia suala la barabara zinazoingia na kutoka katika mtaa huo zinaboreshwa sambamba na kuhakikisha fedha za tasaf zinawafikia wananchi kwani ana dhamira njema na kata ya Mbagala kuu.

Aidha ameahidi kutatua kero za mitaro inayotokea katika mradi wa ujenzi wa mabasi ya mwendokasi unaoendelea katika barabara ya Kilwa ambayo hutiririsha Maji katika barabara ya mtaa wa Kizuiani ambayo imeleta changamoto kadhaa ikiwemo uharibifu wa barabara hiyo.
 

Ameongeza kuwa endapo wananchi watakichagua tena chama cha mapinduzi CCM yeye kama diwani atashirikiana vyema na madiwani wenzake kwenye baraza la madiwani kuhakikisha fedha za mikopo ya asilimia 10 za mapato ya halmashauri zinatolewa kwa wingi kwa wakaazi wa mtaa wa kizuiani na Kata ya Mbagala kuu kwa ujumla.


Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Mbagala Abdala Chaurembo amewaomba wananchi hao kumchagua MAANYA JUMA kuwa diwani ili akawatetee katika baraza la madiwani na kumpa ushirikiano kupitia ofisi ya mbunge huku akiongeza kuwa ndani ya siku 100 za rais SAMIA SULUHU halmashauri ya Temeke  tayari imepewa milion 500 ambapo milion 350 zimepelekwa jimbo la mbagala kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo ya barabara za mtaa wa Kizuiani pamoja na kutenga kiasi Cha milioni 700 kujenga hospitali ya wilaya katika kata ya Chamazi ili kupunguza msongamano katika hospitali ya Temeke.

Akizungumza suala la mikopo ya asilimia Kumi ya Halmashauri,Chaurembo amesema kuwa wao Kama Jimbo la Mbagala wamekuwa wakiwasaidia waombaji wa mikopo hiyo kuandikiwa muhtasari,michanganuo na katiba za vikundi bure zitakazowezesha kupatiwa mikopo hiyo 


Naye mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam Mama CATE KAMBA amesema CCM kupitia rais wa jamhuri ya Muungano  SAMIA SULUHU HASSAN itaendelea kuwaletea maendeleo watanzania na wana mbagala kuu akiwasihi wananchi kukichagua chama hicho huku akiwashangaa wanasiasa wanaobeza maendeleo ya nchi ya Tanzania 

"wananchi wa mtaa wa Kizuiani nawaomba mtuletee kijana wetu huyu Maanya Juma Maanya ambaye ni  mchapakazi ili aende katika Baraza la Halmashauri ya Temeke ili awatumikie vyema kwa kutekeleza ilani ya Chama Cha mapinduzi,CCM yenye kuleta Maendeleao chini ya Mama yetu mpendwa,Rais Samia Suluhu"alisema Bi Cate Kamba

Kampeni hizo pia zilihudhuriwa na wabunge mbalimbali wakiwemo mbunge wa Temeke Doroth Kilave,Mbunge wa viti maalum mkoa wa Dar es salaam Mariam Kisangi pamoja na meya wa manispaa ya Temeke 

Kampeni hizo zimekuja kufuatia kifo Cha aliyekuwa diwani wa kata hiyo,Shabani Othman Abubakar kilichotokea mwezi April mwaka huu ambapo uchaguzi mdogo wa udiwani unatarajiwa kufanyika Julai 18,2021

Comments