SANGENI INTERNATIONAL ILIVYOJIPANGA KUWAUNGANISHA WATANZANIA NA VYUO VIKUU NJE YA NCHI.
SANGENI INTERNATIONAL ILIVYOJIPANGA KUWAUNGANISHA WATANZANIA NA VYUO VIKUU NJE YA NCHI.
Na Thadei Praygod
Dar es salaam.
Katika kuhakikisha wanaokwenda kupata elimu nje ya nchi wanapata elimu bora na ya viwango vya kimataifa ,Wakala wa elimu ya vyuo vya nje ya nchi Sangeni International inayosaidia wanafunzi wanaotazamia fursa za kusoma nje ya nchi inawakaribisha wanafunzi wanaotaka kujiunga na vyuo vya elimu nje ya nchi kutembelea banda lao katika maonyesho ya 16 ya vyuo vya elimu ya juu yanayoendelea katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Afisa habari wa kampuni hiyo Bw. Mzee Mandawa imeeleza kuwa wanafunzi watakaotembelea banda hilo watapata frusa ya kuzifahamu kada mbalimbali zinazotolewa na vyuo vikuu nje ya nchi.
Aidha Kampuni hiyo imekuwa ikiwaunganisha wanafunzi raia wa Tanzania na vyuo mbali mbali duniani haswa haswa vile vyenye kutoa ofa za punguzo la ada hadi asilimia 50 na zenye uhusiana na vyuo vikuu vya nchini India.
“Katika Maonesho haya ya 16 ya Elimu ya Vyuo Vikuu 2021 yanayofanyika kuanzia 26 mpaka 31 Julai katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Sangeni International ikishirikiana na MANIPAL ACADEMY of HIGHER EDUCATION DUBAI CAMPUS kupitia shughuli hii ya maonyesho chuo kinatoa punguzo la ada ya mwaka asilimia 30 kwa wanafunzi mwaka wa kwanza na asilimia 25 kwa digrii ya pili kwa wale tu watakaojisaji na chuo” Taarifa hiyo imeeleza.
Hata hivyo Wanafunzi hao pia watapata tiketi ya ndege kuelekea mji wa Dubai na watapokelewa uwanja wa ndege na kufikishwa kwenye malazi ya chuo na watalipiwa bima ya afya kubwa kwa mwaka wa kimasomo wa mwanzo.
Sangeni International pia itahakikisha ikishirikiana na chuo kuwa wanafunzi wanapata kazi za muda za kulipwa wakati wakiwa masomoni Dubai kwa kuwakabidhi vibali au vyeti vya “No Object Certificate” (NOC).
Kwa mahitaji ya vyuo bora nje ya nchi Kampuni ya Sangeni Internation inakurahisishia ndoto ya kusoma nje ya nchi kuwa kweli hivyo wasiliana na Bw. Ramadhani Chomoka, Mkurugenzi Mkuu – SANGENI INTERNATIONAL, Bw. Peter Galeh, Afisa Usajili Mtendaji (Kanda ya Africa) – MANIPAL ACADEMY of HIGHER EDUCATION DUBAI CAMPUS pamoja na Bw. Mzee Mandawa (Afisa Habari – Sangeni International) Namba: +255(0)784-335-223 Barua Pepe: mzeemandawa@hotmail.com
Tovuti: www.sae.co.tz
Comments