TAMASHA LA 12 LA KITAALUMA LA KIGODA CHA MWAL NYERERE 2021 LAFUNGULIWA DAR
TAMASHA LA 12 LA KITAALUMA LA KIGODA CHA MWL NYERERE 2021 LAFUNGULIWA DAR
Na mwandishi wetu,Dar es salaam
Imeelezwa kuwa licha ya Nchi za Bara la Afrika kuendelea kufanya juhudi za Maendeleo lakini bado inakabiliwa na sera zisizo Madhubuti ikiwemo Utaratibu wa maendeleo,Miundombinu hafifu ikiwemo mawasiliano hali inayopelekea baadhi ya Nchi Kuyumba kiuchumi.
Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Waziri wa katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi katika Ufunguzi wa Maadhimisho ya Tamasha la 12 la Kitaaluma la kigoda cha Mwalimu Julius K Nyerere lililoandaliwa na Chuo Kikuu Cha Dar es salaam,Kampasi ya Mwalimu Julius K Nyerere ,Mlimani
Amesema kutokana na Umuhimu wa Mchango wa Hayati Mwalimu nyerere katika ujenzi wa Taifa hivyo chuo hicho kikuu kiliamua kufanya Matamasha kila mwaka kumuenzi mambo mema aliyoyatenda kwa Taifa na Afrika kwa ujumla
Sanjari na hayo amesema Viongozi waliopambana na Ukoloni na kuwa na Maono ya kutaka Bara la Afrika kuinuka kiuchumi kwa kuanzisha Jumuiya mbalimbali za Mashishikiano ikiwemo ECOWAS,EAC,SADEC,OAU,COMESA, ili kusaidi kuondokana na kuwa temegemezi ili kuwa na Uchumi Imara.
Hata hivyo aliongeza kwa kusema Nchi hizo huzalisha bidhaa zinazofanana kwa ajili ya soko moja la Dunia hivyo kupelekea bidhaa kugongana sokoni na kupelekea bei kushuka
Kwa upande wake makamo mkuu wa chuo,Chuo kikuu cha Dar es salaam Prof Willium Anangisye amesema tamasha hilo la kitaaluma la Mwalimu Nyerere linaikumbusha jamii kuendelea kuwa na ushirikiano madhubuti na limeonyesha matunda makubwa kwa Tanzania,Afrika na duniani kwa ujumla kwa kuenzi historia ya wanamajumuhi wa Bara hilo.
Amesema ni muhimu kuendelea kufanywa kwa matamasha hayo kwani kwani yanaendeleza historia ya umajumuhi wa Afrika na kuwaenzi mashujaa wake.
Hata hivyo licha ya kuwepo kwa changamoto ya ugonjwa wa Corona kwa mwaka huu tamasha hilo limefanyika kwa kufuata tahadhari zote dhidi ya ugonjwa huo



Comments