WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MISITU YA MIKOKO

 WANANCHI WATAKIWA KUTUNZA MISITU YA MIKOKO


Na ThadeiPraygod

Dar es salaam.

Wito umetolewa kwa watanzania hasa wakazi wa wilaya ya Rufiji mkoani Pwani kutoyatumia mashamba ya miti ya mikoko kupanda mpunga kwani kufanya hivyo kunachangia kupotea kwa miti hiyo ambayo ina umuhimu mkubwa katika masuala ya hali ya hewa duniani.

Wito huo umetolewa jijini Dar es salaam na mhifadhi wa wakala wa misitu Tanzania[TFS}Bi Anna Lawuo katika maadhimisho ya siku ya mikoko duniani yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa mradi wa 'TUPANDE  AU TUSIPANDE'unaoratibiwa na shirika la Wetlands Internationa .

Bi Lawuo amesema kuwa siku ya mikoko duniani hufanyika ili kuenzi uhifadhi wa miti ya mikoko ambao huisaidia dunia kupata hewa safi kwani miti hiyo hupunguza kwa kiwango kikubwa hewa ya ukaa yaani carbon.

Ameongeza kuwa ikolojia ya miti hiyo pia husaidia kuzuia upepo wa bahari kwenda nchi kavu kutoharibu kingo za bahari kutokana na uwepo wa mikoko.

Amesema kumekuwa na shughuli za kibinadamu ikiwemo kupanda mpunga na kuvuna chumvi katika miti ya mikoko sambamba na kuitumia kama kuni jambo linalopunguza uwepo wa miti hiyo.

''Mwaka 1961 utafiti ulifanyika hapa nchini na kugundulika kuwepo kwa hekta elfu 53 za mikoko lakini baadaye mwaka 2015 ni hekta elfu 46 tu za mikoko ndiyo zilizokuwepo  hivyo kama serikali tutashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi kuhifadhi mikoko hasa delta ya Rufiji''alisema Bi Lawuo.

 

Naye mkurugenzi wa shirika la Wetlands International kanda ya Afrika mashariki akizungumzia juu ya mradi wa tupande au tusipande uliozinduliwa sambamba na maadhimisho hayo amesema mradi huo utahudumia katika delta ya Rufiji na una lengo la kuiendeleza mikoko kwa kutoa elimu ili wananchi wajue faida za uhifadhi wa miti hiyo


Siku ya Kutunza Mikoko Duniani ambayo ni Julai 26 iliidhinishwa na Mkutano wa Jumla wa Shirika la Elimu ya Kisayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (General Conference of the United Nations Educational Scientific and Cultural Organization) mwaka wa 2015

Comments