Chama cha Soka cha Wanawake champa 'kongole''Rais SAMIA chaahidi Makubwa
Chama cha Soka cha Wanawake champa 'kongole''Rais SAMIA chaahidi Makubwa
Dar es salaam.
Chama
cha soka la wanawake Tanzania (TWFA) kimevitaka vyombo vya habari vya
kitaifa na kimataifa kuacha kuigombanisha na Rais Mama Samia Suluhu
Hassan kufuatia kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kuwa wachezaji wa
timu hiyo wana muonekano kama wanaume.
Akizungumza
kwa niaba ya wachezaji wa timu hiyo, Janeth Christopher alisema kauli
hiyo imetafsiliwa kisiasa na kusababisha mjadala mzito ambao umekua
hauna tija kwa taifa huku akiviomba vyombo vya habari kujadili kauli ya
rais Samia kwa mtazamo chanya, nakuacha kuwagombanisha wachezaji hao na
Rais Samia Suluhu.
Alisema kauli hiyo ilikua
na nia ya kuwapa chachu wachezaji hao ili wafanye vizuri katika
mashindano mbalimbali ya kimataifa na kwamba wataendelea kufanya mazoezi
ya nguvu ili kuendelea kua imara kiafya nakwamba suala la muonekano wao
kama wanaume halitawafanya washindwe kushiriki vyema kwenye michuano.
Awali
Mchezaji Ester Mabanza alisema Rais Samia Suluhu Hassani amekua
mfadhili wao mkubwa tangu akiwa makamu wa rais kipindi cha serikali ya
awamu ya tano ya raisi Dkt. Jonh Magufuli hivyo wataendelea kushirkiana
nae katika kukuza soka la wanawake nchini.
"Mama
Samia ni mama, mlezi na ni Mkuu wa Nchi pia, kwahiyo sisi kutuasa ni
jambo la msingi sana, tumepokea ushauri wake na sisi tutaendelea
kushirikiana nae " alisisitiza Ester Mabanza.
Comments