KWAYA YA ANGAZA SDA,MANZESE YAZINDUA ALBAM YAKE DVD NAMBA 5 'AMENIGUSA' KWA KISHINDO DAR


KWAYA YA ANGAZA SDA,MANZESE YAZINDUA ALBAM YAKE DVD NAMBA 5 'AMENIGUSA' KWA KISHINDO DAR.



Dar es salaam

 Kwaya ya waadventista wasabato ya kanisa la Manzese leo agosti 29,2021 imezindua albam yake namba 5 'AMENIGUSA' na kihudhuriwa na mamia ya waumini wa kanisa hilo na makanisa mengineyo Dar es salaam.


Kwaya hiyo kongwe iliyoanza tangu mwaka 1980 ikiwa na zaidi ya miaka 40 katika uimbaji hapa nchini imezindua kwa kishindo albam hiyo sambamba na kutambulisha rasmi bus lake jipya 'ANGAZA BUS'kama shukrani kwa Mungu  ambalo litatumika kusafirisha kwaya hiyo kuinjilisha katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam,Mikoani na nje ya nchi.

Bus jipya la kwaya ya Angaza SDA,Manzese


Kwaya hiyo iliyohudumu katika matamasha na makanisa ndani na nje ya nchi pia katika nchi mbalimbali ikiwemo katika ikulu ya nchi ya Kenya.


Katika uzinduzi wa albam hiyo ya 'AMENIGUSA'uliofanyika katika viwanja vya kanisa la waadventista wasabato Manzese pia kwaya mbali mbali zimehudumu ikiwemo kwaya ya watoto ya Angaza junior,New Heaven Choir ya kanisa la Moravian,Kwaya ya Tandale SDA,Sauti ya Nyikani,pamoja na Kwaya ya MBIU



Katika uzinduzi wa albam hiyo 'uliofanyika katika viwanja vya kanisa la waadventista wasabato Manzese pia kwaya mbali mbali zilizoalikwa zimehudumu ikiwemo kwaya ya watoto ya Angaza junior,New Heaven Choir ya kanisa la Moravian,Kwaya ya Tandale SDA,Sauti ya Nyikani,pamoja na Kwaya ya MBIU.


Comments