LHRC YAIOMBA SERIKALI KUONGEZA USIMAMIZI,UPATIKANAJI WA HAKI MAHALI PA KAZI.

LHRC YAIOMBA SERIKALI KUONGEZA USIMAMIZI,UPATIKANAJI WA HAKI MAHALI PA KAZI.

 

 


Dar es salaam.

 Serikali imeombwa kuendelea kuhimiza wafanyabiashara, makampuni kufuata haki za binadamu mahali pa kazi naa kuepuka vitendo viovu makazini ikiwemo rushwa,ubaguzi,unyanyaswaji hali itakayopelekea uchumi wa Nchi kutopiga hatua

Ombi hilo limetolewa leo Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Anna Henga katika ufunguzi wa Mdahalo na Sekta ya biashara ambapo amesema ni budi kampuni ijali mazingira ya Wafanyakazi wao kwani wengine hupitia changamoto ikiwemo kulipwa mshahara mdogo,kufanya kazi kwa muda mrefu, masaa 24 bila kupumzika hivyo kupelekea wengine kupata matatizo ya kiafya .

"Ni budi Makampuni kuhakikisha shughuli wanazizifanya kurudisha faida kwa jamii kwa kutoa misaada mbalimbali ikiwemo kununua vifaa mashuleni,hospitali kwani ujenzi wa Nchi lazima wahusike kwani nao hupata faida"alisema Anna Henga

Kwa upande wake Mshiriki katika Mdahalo huo Wilfred Mwakibala amesema Serikali haina budi kutengeneza sheria,taratibu zitakazosaisadia kulinda haki za binadamu  mahali pa kazi

Hata hivyo ameongeza kwa kusema baadhi ya maeneo ya makazi wafanyakazi hawajariwi na hata wanapopata ajali wawapo kazini kupatiwa matibabu ni changamoto kwanihuwa  hawajakata bima wenyewe hivyo serikali haina budi kusimamia sheria za wafanyakazi hao ili usawa na haki upatikane mahali pa kazi

Naye Afisa programu mwandamizi masuala ya utafiti kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC Joyce Komanya amesema kwa mujibu ya ripoti iliyofanywa mwaka 2020/2021 inaonyesha vitendo vingi vya ukiukaji haki za binadamu mahali pakazi vikiwemo ujira mdogo ajira za watoto wadogo mazingira hafifu ya utendaji kazi hali hiyo serikali haina budi kuingilia kati

 

Comments