MREMBO MISS EAST AFRIKA 2021 KUZAWADIWA GARI LA KIFAHARI
MREMBO MISS EAST AFRIKA 2021 KUZAWADIWA GARI LA KIFAHARI
mrembo wa Afrika Mashariki, Miss East Africa 2021 yatafanyika jijini Dar es salaam mwezi wa Novemba mwaka huu.
Makamu
wa Rais wa mashindano hayo, Jolly Mutesi amesema kuwa maandalizi ya
awali ya mashindano hayo makubwa ya urembo yameanza na kuwataka warembo
kuanza kujiandaa ambapo mshindi atazawadiwa gari la kifahari aina ya Nissan.
Alisema kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kuangaliwa
na watu wengi Dunia nzima kupitia kwenye matangazo ya moja kwa moja ya
Televison (Live) na hivyo kutoa nafasi nzuri ya kutangaza utalii wa
Tanzania pamoja na kuonyesha fursa mbalimbali za uwekezaji
“Hii ni
fursa kwa makampuni mbalimbali yanayohitaji kutangaza biashara zao kwa
ndani nan je ya mipaka ya Tanzania kupitia katika mashindano haya
makubwa ya urembo,” alisema Mutesi.
Alisema kuwa jumla ya nchi 16
zitashiriki katika mashindano haya. Nchi hizo ni ambazo ni Kenya,
Uganda, Rwanda, Burundi, Ethiopia, Eritrea na Djibouti.
Nchi nyingine ni Somalia, Madagascar, Malawi, Seychelles, South Sudan, Comoros, Reunion na Mauritius.
Mashindano
ya Miss East Africa yalianzishwa na Mtanzania Rena Callist na
kufanyika kwa mara ya kwanza mwaka 1996 kwa mafanikio makubwa katika
Hoteli ya Sheraton (Serena kwa sasa).
Mashindano hayo pia yamewahi
kufanyika katika nchi ya Burundi kwa udhamini wa Rais wa Burundi wa
wakati huo hayati rais Piere Nkurunzinza
Mashindano ya mwisho
kufanyika ilikuwa ni mwaka 2012 ambapo yalifanyika katika ukumbi wa
Mlimani City Jijini dar es salaam na kuangaliwa na mamilioni ya watu
Duniani kote kupitia matangazo ya moja kwa moja mubashara ambapo
yalitangaza utalii wa Tanzania kwa kiasi kikubwa.
Alisema kuwa
kuanzia sasa mashindano ya Miss East Africa yatakuwa yakifanyika kila
mwaka ambapo yatasaidia sana katika kudumisha umoja wa Afrika mashariki.
Pia
mashindano haya yatasaidia kukuza utalii, kutangaza fursa mbalimbali za
uwekezaji hasa katika nchi inayoandaa mashindano hayo na pia kutoa
elimu na kusaidia katika changamoto mbalimbali hasa zinazowakabili
wanawake na watoto wa ukanda huu wa Afrika ya Mashariki.
Mashindano hayo yanaandaliwa na kampuni ya Rena Events Limited ya Jijini Dar es salaam, Tanzania.
Comments