NEW MARHABA CATERING YAJIVUNIA UPISHI BORA WA VYAKULA DAR

 NEW MARHABA CATERING YAJIVUNIA UPISHI BORA WA VYAKULA DAR 

 

DAR ES SALAAM.

Kampuni ya mapishi katika shughuli mbalimbali ya New  Marhaba Katering imewataka watanzania kuitumia kampuni hiyo katika shughuli zao za harusi,kitchen party,kiofisi na nyinginezo za kulisha wageni mbalimbali.

Hayo yalisemwa jijini Dar es salaam na Mwanzilishi wa kampuni hiyo Bi lulu Omar alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika shughuli ya uzinduzi wa jezi mpya za Klabu ya Yanga ambapo New Marhaba ilikuwa kampuni iliyohudumia vyakula katika sherehe hizo.

Bi Lulu alisema kuwa anaishukuru klabu ya soka ya Yanga kwa kuona ana uwezo mkubwa wa kulisha viongozi mbalimbali wa klabu hiyo,wageni mbalimbali mashuhuri namashabiki waliohudhuria katika sherehe za uzinduzi wa jezi za klabu ya Young Africans kwa msimu wa ligi kuu nchini kwa mwaka 2021/2022.

''naishukuru sana klabu ya Yanga kwa kuona kuwa kampuni Yangu inastahili kupika na kulisha watu katika shughuli hii ya leo na watu wengi wamefurahia chakula chetu kwani tunapika chakula kitamu na kizuri na upishi miminilifundishwa na marehemu Mama yangu mzazi kutoka Zanzibar na kwa kuwa nilikuwa naupenda upishi nikajikuta naanza kupika katika mashughuli mpaka leo hii''alisema Bi Lulu.

Aidha amewataka wananchi wa jiji la Dar es salaam wenye shughuli zinazohitaji chakula kuitumia kampuni ya New Marhaba Katering ili waifurahie ladha nzuri ya chakula na chenye ubora.

Wanaohitaji huduma za chakula kwenye sherehe mbalimbali kwa bei nafuu kutoka NEW MARHABA wanaweza kumtafuta Bi Lulu Omar kwa namba 0653 11 08 67 au kufika katika ofisi zao eneo la Chang'ombe wilayani Temeke mkoani Dar es salaam.


Comments