SHIRIKA LA NURU YETU FOUNDATION LAWAKUTANISHA WADAU MBALI MBALI KWENYE ''GIRLS ROUNDTABLE''
SHIRIKA LA NURU YETU FOUNDATION LAWAKUTANISHA WADAU MBALI MBALI KWENYE ''GIRLS ROUNDTABLE''
Dar es Salaam
Taasisi ya Nuru yetu Foundation imewataka vijana mbalimbali hususani wanawake kushiriki katika semina mbalimbali zinazoendeshwa na Taasisi hiyo kupitia (Girls Round Table ) kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali kupitia kwa watu waliofanikiwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo, Zauja Mohamed amesema kuwa, pamoja na mambo mengine lengo la Taasisi hiyo ni kuwaenua wanawake hususani vijana kuweza kujifunza kupitia watu maarufu ambao wamefanikiwa.
"Hii girls round table huu ni msimu wetu wa nne ambapo tunawashirikisha wadau mbalimbali kutoa elimu kwa vijana wetu ambao wana nia ya kufanikiwa ambapo mada mbalimbali zinakuwa zinajadiliwa ikiwepo, ulemavu, ukimwi, afya, vipaji pamoja na Sanaa kupitia watu waliofanikiwa"amesema Zauja.
Aidha amesema pia Taasisi hiyo imeanzisha kampeni ya Mama yangu, Malkia wangu, lengo likiwa ni kuwasaidia single mother ambao wanalea watoto wao katika mazingira magumu mno ili kuweza kuwapa hamasa ya kuwapatia vitu mbalimbali ambayo vitaweza kumsaidia mtoto kufikia ndoto zake.
Kwa upande wake, Masoud kipanya ambae ni miongoni mwa wzungumzaji katika semina hiyo, amewataka vijana kusimamia na kutimiza katika ndoto zao kwa vitendo ili waweze kufikia malengo yao, huku akiitaka jamii kuwafichua watoto wenye ulemavu ili waweze kupata misaada ikiwemo elimu.
Malaika ni msanii wa kizazi kipya, kwa upande wake, amewataka vijana kujitambua na kupigania ndoto zao kwani hakuna mafanikio ambayo hayana changamoto, muhimu ni kujiamini katika kile unachokiona kinafaa na ukakiendeleza huku akiwataka wazazi na walezi kuwasapoti watoto wao pale wanapokua wanafanya jamabo.
Naye, Baby John Musamba ambae ni Mwenyekiti muanzilishi wa Taasisi Tanzania voiceof humanity inayosimamia na kueka mustakabal na ustawi wa watu wanaozaliwa na(Jinsi Tata) ameiomba Serikali kuwatambua watu hao pamoja na kuchukua hatua kwa watu wenye ulemavu ambao hauonekani ikiwemo kuwatengezea sera zao pamoja na kuwatenganisha katika makundi ili iwe rahisi kuweza kusema changamoto zao.
Comments