SHULE YA BETHELI MISSION ACADEMY YAJIVUNIA KITAALUMA,YAWATAKA WAZAZI/WALEZI KUENDELEA KUIAMINI. Dar es salaam.
SHULE YA BETHELI MISSION ACADEMY YAJIVUNIA KITAALUMA,YAWATAKA WAZAZI/WALEZI KUENDELEA KUIAMINI.
Shule ya Bethel Mission Academy iliyopo Makuburi, Wilayani Ubungo jijini Dar es Salaam imewataka wazazi na walezi ambao wanasomesha waatoto katika shule hiyo kuendelea kujenga imani na uongozi wa shule kwani wamejipanga vya kutosha kuhakikisha wanafunzi wanaofanya mtihani wa darasa la saba wanafaulu kwa kiwango cha juu.
Rai hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwalimu wa Taaluma wa shule hiyo, Jeremia Nyandigisi,wakati akifanya mahojiano na Mtandao huu, ikiwa zimebaki siku chache kufanyika kwa mtihani wa Taifa wa darasa la saba, ambapo amesema imeshafanya maandalizi ya kutosha kwa wanafunzi hao na kujiridhisha wapo vizuri hivyo kilichobaki ni kusubiria mtihani tu.
Amesema kuwa, wamekua wakifanya mikakati mbalimbali ya kuwasaidia wanafunzi hao kuweza kufanya vizuri ambapo wamekua wakiwapima kwa kuwaandalia mitihani mara kwa mara pamoja na kuwashindanisha na shule mbalimbali kutoka mikoa tofauti tofauti ikiwemo Dodoma, Iringa, Mbeya, Morogoro pamoja na Kagera ambapo wanafunzi hao wameweza kufanya vizuri sana.
"Tumejipanga vizuri sana kuhakikisha wanafunzi wetu wote wanakuwa bora kitaifa na kitaaluma kwa kukidhi viwango vyote vya kimasomo na mitihani, tunatumia njia nyingi kuwapima wanafunzi wetu, wamekua bora sana na maadili"amesema Jeremia.
Ameongeza kuwa katika kuelekea mtihani wa darasa la saba kwa mwaka 2021 shule hiyo imekuwa ikiwaandaa vyema wanafunzi kwa kuhakikisha wanakuwa na uelewa wa masomo yote pamoja na kufanya mitihani mbalimbali ya kujipima ndani ya shule na nje ya shule kwa kushiriana na shule nyingne mbalimbali za ndani na nje ya mkoa wa Dar es salaam.
"Tumefanya mitihani kwa kushirikiana na shule ya shule kama Lusasaro ya kisukuru na Remnant ya Tabata,tumejiridhisha wanafunzi wetu wapo vizuri sana matokeo yao yamekua yakiridhisha kwani hatuwaandai tu kwa ajili ya mitihani pekee bali kitaaluma kwa ujumla, pia kwa mwaka huu tumejipanga kufanya mahafali kwa kufuata taratibu zote zilizowekwa na Serikali"amesema Nyadigisi.
Hata hivyo ameongeza kuwa katika suala la Imani shule imekuwa ikiwa ni kipindi cha maombikila asubuhi ili kuwajenga wanafunzi kiimani na kumjua zaidi mwenyezi Mungu sababu inayowatofautisha na shule nyingine hapa nchini na kuwaongezea upeo wanafunzi wao kumjua Mungu na masomo kwa ujumla na kuwakaribisha wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika shule hiyo.
Comments