Miaka 5 ya anezylita desing yaja na duka jipya la mapambo, mafunzo ya mapishi
Miaka 5 ya anezylita desing yaja na duka jipya la mapambo na mapishi
Jamii imeombwa kutumia vizuri mitandao ya kijamii kwa kujifunza mambo mbalimbali ambayo yanaweza kuwasaidia katika maisha yao.
Rai
hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Anezylita Bi. Zena
Shariff Scaba wakati wa uzinduzi wa duka lake jipya ambalo linajihusisha
na masuala ya mapambo ya nyumbani pamoja na shule ya mapishi ya keki.
Kampuni
hiyo ambayo ilikua inafanya mashindano ya kupika keki ambapo mwaka jana
na mwaka huu hayajafanyika kutokana na ugonjwa wa korona, ambapo
mashindano hayo yataanza hivi karibuni.
Bi
Zena amewambia wanahabari kwamba vijana waliopo nyumbani watapata
mafunzo ya mapishi na kupatiwa vyeti vya serikali ya Tanzania hivyo
amewataka wachangamkie fursa hiyo.
"Tumeamua
kufungua duka jingine ili vijana wajifunze mapishi lakini pia kuuza
mapambo ya majumbani kwa gharama nafuu sana, wananchi wajitokeze kutumia
fursa hii" amesema Bi Zena.
Aidha amesema kuwa
kampuni yake imewezesha kutoa ajira kwa vijana wengi wa kitanzania
ikiwa ni sehemu ya kuiunga mkono serikali katika kukabiliana na
changamoto ya ukosefu wa ajira.
Hata hivyo
ameiomba jamii itumie vizuri mitandao ya kijamii kujifunza mambo
mbalimbali pamoja na kutumia kama njia ya kutangaza biasha zao.
Comments