MSHINDI MISS TANZANIA EASTERN ZONE KUZAWADIWA KITITA.
MSHINDI MISS TANZANIA EASTERN ZONE KUZAWADIWA KITITA.
Dar es
salaam.
Lile
shindano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa tasnia ya urembo
kanda ya Mashariki lijulikanalo kama Miss Tanzania Eastern Zone linatarajiwa lifanyika septemba 24 mkoani Morogoro.
Akitoa
taarifa ya fainali za shindano hilo
mbele ya wanahabari jijini Dar es salaam,Mkurugenzi wa kampuni ya Tips
Forum Mhandisi Nancy Matta ambao ndiyo waandaaji na waratibu wa shindano hilo
amesema maandalizi yake yamekamilika kwa kiasi kikubwa ambapo mshindi wa
mashindano hayo atawakilisha katika mashindano ya kitaifa ya Miss Tanzania.
Amesema kuwa
mashindano hayo yalianza ngazi za mikoa katika mikoa ya Lindi,Mtwara,Pwani na
Morogoro na kupatikana washindi 16 ambao watashiriki katika fainali ngazi ya
kanda ya Mashariki.
Ameongeza
kuwa mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika katika hoteli ya Morena mkoani humo
ambapo mshindi wa kwanza atapata kitita cha shilingi milioni 2,mshindi wa pili
sh milioni 1.5 na mshindi wa tatu
atajinyakulia kitita cha sh milioni 1.
Aidha amesema
kuwa lengo la kuanzisha mashindano hayo ni kukuza sekta ya urembo hapa nchini
na kuutangaza utalii ndani na nje ya nchi kupitia mashindano hayo.
Nao baadhi
ya wadhamini wa mashindano wakiwemo bodi ya Taifa ya utaliii TTB ambayo
imewakilishwa na BI Maria Mafie ambaye amesema bodi hiyo imeamua kudhamini
mashindano hayo ili kuendelea kukuza sekta ya utalii ndani na nje ya nchi
kupitia mashindano ya ulimbwende.
Kwa upande
wake Meneja mauzo wa hoteli ya Serena Shaban
Kaluse amesema mashindano hayo yatakuwa chachu ya kuutangaza utalii wa
Tanzania.
Naye Niwako
Charles ambaye ni afisa masoko hoteli ya Dynasty Beach ambapo washiriki wa
kinyanganyiro hicho wameweka kambi katika hoteli hiyo amesema kuwa wataendelea
kuunga mkono mashindano hayo ambayo yatatoa mlimbwende atakayeiwakilisha kanda
ya kati katika mashindano ya Miss Tanzania.
Mashindano
hayo yamedhaminiwa na makampuni mbali mbali ambapo mdhamini mkuu ni chanel ya
utalii ya Taifa kupitia shirika la utangazaji
Tanzania ,[Tanzania Safari Channel].
Comments