Skip to main content

Mwenyekiti Pazi azindua Bonanza la Kipunguni Smart Bonanza.

 

Mwenyekiti Pazi azindua Bonanza la Kipunguni Smart Bonanza.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Wilaya ya Ilala Ndugu Hamadi Pazi amezindua Bonanza la Kipunguni Smart Bonanza lililo andaliwa na Bar ya Smart iliyopo Banana pamoja na Ofisi ya Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Kipungunj Kata ya Kipawa Jijini Dar es salaam.

Bonanza hilo limelenga kuviunganisha vikundi vya Jogging pamoja na kuhamasisha ufanyaji wa mazoezi mara kwa mara ili kusaidia kuimarisha Afya.

Aidha Bananza hilo limeenda sambamba na zoezi la uchangiaji wa damu kwaajili ya kuokoa maisha ya Wagonjwa wenye uhitaji wa damu.

Aidha Ndugu Hamadi Pazi ametoa pongezi kwa waandaaji wa Bonanza hilo Uongozo wote wa Smart pamoja na Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Kipunguni chini ya Mwenyekiti ndugu Mwijuma Seke.

Hata hivyo Mwenyekiti Pazi amewapongeza vijana wote walio jitoa katika zoezi la uchangiaji wa damu ambayo itasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa hospitalini pamoja na uwepo wao katika Bonanza hilo.


d

Comments