TADB yatoa mkopo wa milioni 436 ujenzi kiwanda kusindika korosho Tanga
TADB yatoa mkopo wa milioni 436 ujenzi kiwanda kusindika korosho Tanga
Na Mwandishi Wetu, Tanga
Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeidhinisha mkopo wa kiasi cha
shilingi 435,500,000/- kwaajili ya uanzishwaji wa kiwanda kidogo cha
kusindika korosho ili kuliongezea thamani zao sambamba na kuongeza pato
la taifa pamoja na kuinua pato la mkulima..
Akizungumza na
waandishi wa habari mara baada ya uzinduzi wa mradi wa Ubunifu katika
mnyororo wa thamani wa zao la Korosho chini ya Taasisi ya Care Tanzania
wilayani Mkinga,Jijini Tanga, Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TADB,Bw
Jeremiah Jeremiah Mhada alisema kuwa benki hiyo imeidhinisha mkopo
huoambapo zitatumika katika ujenzi wa kiwanda na ununuzi wa mashine na
vifaa mbalimbali za kuendesha kiwanda hicho.
“Fedha hizo zitatoka
kwa awamu ikiwa ni kujenga miundombinu ya kiwanda na awamu ya pili
kufadhili wakulima wa korosho pembejeo zitakazowawezesha kuzalisha
korosho kwa tija na kupata bei nzuri sokoni,” alisema Bw.Mhada
Alieleza
kuwa fedha ziizotolewa zitakwenda kusaidia katika kutengeneza ajira
kupitia kazi ya ujenzi wa majengo ya kiwanda pia kukiwezesha kiwanda
Mtaji wa kununua korosho kutoka kwa Wakulima wadogo wa Kilimo Viwanda
Sigaya Limited.
“TADB imetoa mkopo huu kwa lengo la kuongeza
thamani ya zao la korosho hali itakayopelekea kuongezeka kwa mapato ya
wakulima wa korosho Wilayani Mkinga, alisema Bw.Mhada na kuongezea kuwa
kiwanda hicho kitaongeza thamani ya zao na kuhamasisha wakulima kufanya
kilimo cha korosho kutokana na uhakika wa soko.
Bw .Mhada
alisisitiza kuwa majukumu ya TADB ni kuhakikisha mageuzi yanafanyika
katika sekta ya kilimo na kuwabadilisha wakulima kutoka kilimo cha
mazoea na kufanya kilimo biashara na kuwafanya waweze kupita hatua
kiuchumi kupitia shughuli za kilimo na kuwaunganisha na masoko kupitia
chama cha msingi cha ushirika cha DUGA.
“Uchakataji wa korosho
hapa nchini utasaidia kuzalisha bidhaa nyingine kama mafuta kwa asilimia
15 ambayo hutumika kama dawa na matumzi ya viwandani jambo
litakalopelekea kuongeza thamani ya zao la korosho hapa nchini,” alisema
Alieleza
kwa sasa mafuta ghafi ya korosho yanauzwa katika soko la Umoja wa
Ulaya, Marekani, Japan, Korea ambapo wasambazaji wakuu ni India na
Brazil. Hivyo tukiweza kuzalisha wenyewe mafuta haya Tanzania itakuwa
miongoni mwa wasambazaji wakuu wa bidhaa hiyo Duniani.
“Kwa
mujibu wa ANSAF mwaka 2016/17 Tanzania ni namba 3 kwa uzalishaji wa
korosho Duniani, sasa hivi ipo namba 4 kwa Afrika ambapo zaidi ya
asilimia 90 inasafirishwa kama malighafi,” alisema Bw.Mhada
“TADB
tutaendelea kuhamasisha kuongeza na kukuza uzalishaji nah ii ni
muendelezo wa uwekezaji wa zaidi ya bilioni 33 ambazo zimetolewa katika
mnyororo wa thamani wa uzalishaji, alieleza Bw.Mhada
Mwenyekiti
wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha DUGA, Bw.Said Hassan Tuwano
aliishukuru benki ya TADB pamoja na Wawekezaji walioamua kuwekeza katika
Wilaya yao na kusema hii imeonyesha dhamira ya dhati ya kusaidia
wakulima wadogo nchini.
“Nashukuru zaidi kwa kutupa asilimia 45
ya hisa kwenye kiwanda hivyo zaidi ya wakulima 200 tutakuwa sehemu ya
kiwanda na tumejipanga kuhakikisha tunaongeza idadi ya wakulima mpaka
kufikia 2,500 katika Wilaya yetu ili tunufaike wote,” alisema Bw.Tuwano
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Kanali Maulid Surumbu aliwataka
wadau wote kutekeleza majukumu yao kuhakikisha uzalishaji wa zao la
korosho unaongezeka pia kuhakikisha kiwanda kinakamilika ili uzalishaji
uanze msimu ujao wa mavuno.
“Tunachotaka kutoka kwenu ni uwazi na
uwajibikaji, niwahakikishe Serikali ipo pamoja na nyinyi kutoa mchango
ili kuhakikisha tija katika uzalishaji inaongezeka na kufanya korosho
yetu izidi kukubalika katika soko la ndani na masoko ya kimataifa jambo
litakalo ongeza kipato kwa wakulima Wilayani Mkinga,” alisema Kanali
Surumbu.
Comments