[UCSAF] YAKUTANA NA WATOA HUDUMA ZA MAWASILIANO,YAOMBA USHIRIKIANO KUKUZA SEKTA HIYO.
[UCSAF] YAKUTANA NA WATOA HUDUMA ZA MAWASILIANO,YAOMBA USHIRIKIANO KUKUZA SEKTA HIYO.
![]() |
DAR ES SALAAAM
Katika jitihada za serikali kukuza sekta ya mawasiliano ambayo ni chachu ya maendeleo ya Taifa lolote ulimwenguni,Mfuko
wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) umewaomba watoa huduma za mawasiliano
wa sekta ya umma na binafsi kushirikiana na mfuko huo ili kuhakikisha
kuwa huduma za mawasiliano zinawafikia watu wote nchini bila kuwa na vikwazo vya ufikaji wa huduma hiyo kwa kiwango cha juu.
Akizungumza jijini Dar es salaam na wadau wa sekta ya mawasiliano katika mkutano uliyoandaliwa na kuratibiwa na mfuko huo Afisa sheria mwandamizi wa mfuko
huo Fredy Kandonga amesema
ili huduma ya mawasiliano iweze kufika maeneo yote yanayohitaji huduma
hiyo ni vyema kuwa na ushirikiano madhubuti wa watoa huduma.
Aidha
ameseongeza kuwa bado kuna changamoto ya upatikanaji wa huduma ya mawasiliano
katika maeneo ya mipakani na vijijini jambo ambalo linawafanya wananchi wa maeneo hayo ya mipaka watumie
huduma za mawasiliano za nchi jirani na maudhui ya nchi hizo jambo linalokwamisha ukuaji wa uchumi kwa kiasi fulani.
Hata
hivyo amesema katika jitihada za kuhakikisha kuwa elimu ya mfuko huo wa
mawasiliano inawafikia watu wengi wamekuwa wakifanya mikutano ya wadau
wa mawasiliano katika maeneo mbalimbali ikiwemo mikoa ya Dodoma, Mbeya,
Mwanza na Arusha pamoja na kufanya vipindi vya elimu kwa umma kupitia
vyombo vya habari ambapo pia katika hatua nyingine mpaka sasa wameshafikisha huduma za mawasiliano zaidi ya
maeneo 1064.
''Wakati Mfuko unaanza takriban asilimia 45
tu ya watanzania walikuwa wanaishi katika maeneo yanayofikiwa na
mawasiliano ya simu. Mpaka tunavyoongea leo takriban asilimia 94 ya
watanzania wanaishi kwenye maeneo yanayofikiwa na mawasiliano ya simu
ambapo zaidi ya asilimia 70 ni watumiaji wa huduma za mawasiliano ya
simu. Asilimia 10 imechangiwa na Mfuko wa Mawasiliano''alisema Bw Kandonga.
Kwa upande
wake Mhandisi Shirikisho Mpunji kutoka idara ya uendeshaji ya mfuko huo
amesema mwaka 2006 kabla mfuko kuanzishwa kulikuwa na changamoto nyingi za upatikanaji huduma za mawasiliano lakini mfuko huo kupitia mradi wake mkubwa wa mawasiliano vijijini ulitanua wigo wa mawasiliano ambapo mpaka sasa maeneo mengi yanapata huduma za mawasiliano kwa kushirikiana na serikali na sekta binafsi.
![]() |
Mhandisi Shirikisho Mpunji akiongea na wanahabari [hawapo pichani]
Serikali ilianzisha Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote mwaka 2006kupitia sheria ya bunge namba 11 ya mwaka 2006 sura ya 422 na kusainiwa na Mheshimiwa Raisi mwaka 2007. Hata hivyo kanuni za kuanzisha Mfuko zilisainiwa Aprili 2009. Lengo kuu la kuanzishwa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote ni kuhakikisha Mtanzania popote alipo ataweza kupata huduma za uhakika za mawasiliano iwe ni mawasiliano ya simu za mkononi, utangazaji, huduma za posta au intaneti.
Toka kuanzishwa kwake Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote umejikita kutambua mahitaji ya mawasiliano nchi nzima, kushirikisha wadau mbali mbali wa mawasiliano nchini, kushirikisha wananchi katika kutambua na kutatua kero za mawasiliano.




Comments