UDSM YADHAMIRIA KUANZISHA MAFUNZO MAALUM YA TIBA ZITOKANAZO NA NYUKI NA MAZAO YAKE

 

UDSM YADHAMIRIA KUANZISHA MAFUNZO MAALUM YA TIBA ZITOKANAZO NA NYUKI NA MAZAO YAKE


***********************

Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Kimedhamiria ndani ya mwaka mmoja kuazisha Mafunzo Maalum ya tiba zitokanazo na nyuki na mazao yake.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki hii mkoani Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kituo cha Matibabu kwa kutumia Nyuki na Mazao yake ( TANZANIA INTERNATIONAL BEE CO. )Kilichopo Sinza Mkoani hapo.

Akizungumza katika uzinduzi huo mwalimu wa chuo Kikuu cha Dar es Salaam Daktari Mkambwa Manoko amesema, kwa kuwa nchi ya Tanzania ni ya pili Afrika katika uzalishaji wa Nyuki wameona kuna haja ya kuanzisha mafunzo hayo yatakayomuwezesha Mtanzania Kuelimika na yatokanayo na nyuki na mazalia yake.

Kwa upande wake meneja wa rasilimali za nyuki toka wakala wa huduma za misitu Tanzania ( TFS) Hussein Msuya akizungumza katika uzinduzi huo amesema kupitia kituo hicho mbali na kutoa huduma ya Afya , kutawezesha kupanua zaidi rsilimali za nyuki na kupanua myororo wa thamani zao hilo.

Aidha kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi kutoka kituo hicho cha TANZANIA INTERNATIONAL BEE CO. LTD Peter Mayunga na Mtaalamu wa Matibabu kwa kutumia Nyuki na Mazao yake Musiba Poul Kiteba wamesema kituo hicho ni cha kwanza hapa nchini huku wakijikita zaidi katika utoaji wa elimu ya ufugaji wa nyuki pamoja na Matibabu kwa kutumia Nyuki na Mazalia yake.

Sanjari na hayo Mtarajio ya Bodi ya Kituo hicho cha Matibabu yatokanayo na Nyuki na Mazalia yake ni kuanzisha zaidi ya vituo thelasini nchi nzima mpaka mwaka 2023.

Comments