UONGOZI WA SERIKALI YA MTAA WA BONYOKWA, WAISHUKURU HALMASHAURI YA JIJI LA DSM

 

UONGOZI WA SERIKALI YA MTAA WA BONYOKWA, WAISHUKURU HALMASHAURI YA JIJI LA DSM

 Dar es Salaam.

Uongozi wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa kwa kushirikiana na Kikundi cha Makazi Group wameipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia mkopo wa shill mill 210.
Aidha, uongozi wa kikundi cha Makazi umempongeza Mwenyekiti wa Mtaa huo, Shabaan Maliyatabu kwa kuwapatia msaada wa hali na mali mpaka kufanikisha zoezi la kupata mkopo huo na kuwahidi kuwapa mashirikiano, huku akitaka vijana wachangamkie fursa hiyo. 

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa Shaaban Maliyatabu amesema fedha hizo zimetoka katika mkopo wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambao unatolewa bila riba, huku ikiwa 
umelenga kuinua shughuli za maendeleo kwa jamii.

Amesema kuwa, kikundi hicho kina jumla ya watu 12 ambao wamesajili kikundi chao na kufuata tararibu zote, na kufanikiwa kupata mkopo huo wa kuanzishia mradi huo.
Aidha, amesema kupitia fedha hizo wameanzisha  mradi  mkubwa wa ufyatuaji matofali na duka la vifaa vya Ujenzi ikiwemo mbao, mchanga, matofali na taa ambapo mradi huo upo karibu na Bonyokwa stend kuelekea Segerea.

Aidha, amesema pia wameweza kunuua magari matatu kwa ajili kuendeshea kikundi hicho pamoja na kutoa ajira ambapo magari hayo yatatumika kwa ajili ya shughuli za usafirishaji.

Amesema kuwa, vijana mbalimbali ndani ya Mtaa huo wamehamasika na kuunda vikundi vya kijamii, kiuchumi na uzalishaji mali kikiwemo Makazi Group,

Hata hivyo, amewataka kuitunza miradi hiyo ili iweze kuleta maendeleo makubwa ya kuweza kujiendesha wenyewe na kuweza kurudisha mikopo hiyo na wengine waweze kufaidika kama lilivo lengo la Serikali.

Comments