4121 wahitimu UDSM,KiKWETE Aupongeza Uongozi wa Chuo Kwa Kupiga Hatua Katika Usawa wa Jinsia Kwa Wahitimu
4121 wahitimu UDSM,KiKWETE Aupongeza Uongozi wa Chuo Kwa Kupiga Hatua Katika Usawa wa Jinsia Kwa Wahitimu
Mkuu
wa Chuo Kikuu Cha Dar es salaam (UDSM) Rais Mstaafu mhe. Jakaya Mrisho
Kikwete ameupongeza uongozi wa chuo hicho kwa kupiga hatua katika usawa
wa jinsia kwa wahitimu wa shahada za waliohitimu chuoni hapo mwaka huu
wa masomo 2021.
Pongezi hizo amezitoa wakati
akiwatunuku vyeti wahitimu wapatao 4121 wa awamu ya pili katika ngazi
ya digrii akisema kuwa amefurahishwa na idadi ya wanafunzi wa kike
kuongezeka mwaka hadi mwaka na kuutaka uongozi wa UDSM kuhakikisha usawa
wa kijinsia kwa wahitimu unafikia asilimia 50 kwa 50.
"Nimesikiliza
hotuba yako Makamu mkuu wa chuo nimefurahishwa na takwimu kwamba
wahitimu wote wapo 4121 lakini kati ya wanaume ni 2101 na wanawake i
1920, hatua hii ni nzuri sana, usawa wa kijinsia kwa wahitimu wa shahada
za awali unaonekana kupanda hivyo nawapongeza sana kwa hatua hiyo,"
alisema Dkt. Kikwete.
Awali
Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dr. William Anangisye amesema kwamba chuo
hicho kimepata mafanikio makumbwa ikiwemo kupata kiasi cha Billioni 3
kwa ajili ya kufanya utafiti na ubunifu,pamoja nakuanza kudahili
wanafunzi kutoka mataifa yakigeni kwa ajili yakujifunza lugha ya
kiswahili.
Hata hivyo Profesa Anangisye
amewaasa wahitimu hao Kuwajibika kwa kutumia elimu zao kuwa na ushawishi
wa kuleta chachu ya maendeleo katika Taifa na Dunia kwa ujumla, kufanya
kazi kwa bidii, pamoja na kuendelea kujifunza mambo mapya na sio kubaki
nyuma.
"Tuna wapongeza sana mnaohitimu leo,
lakini napenda niwakumbushe msiende kutegemea kuajiriwa serikalini,bali
mkawe chachu yakutengeneza ajira, mfanye kazi kwa bidii, muwe na nidhamu
kazini, mjiendeleze kimaarifa lakini pia mkipata nafasi za kazi za
kujitolea mfanye ili mjijengee uzoefu nankujiami, kwahiyo msikate tamaa
mnapokumbana na changamoto mbalimbali za kazi" amewaasa Profes huyo.
Nae
Mwayekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es salaam ( UDSM) Jaji
Mstaafu Damian Lubuva ameshukuru hatua zinazo chukuliwa na Rais Samia
kujikinga na uginjwa wa Uviko 19, nakutumia fursa hiyo kusema kuwa chuo
kinaendelea kuzingatia maelekezo ya wataalamu wa afya.
"Nyinyi
wahitimu na wale mnaobakia nawaomba muendelee kuchukua tahadhali kama
tunavyoelekezwa na wataalamu wa afya kuhusu ugonjwa wa uviko 19, rais
amekuwa mstari wa mbele kutukumbusha haya na sisi tuendelee kumuunga
mkono" amesema Jaji Mstaafu Lubuva.
Jumla
ya wahitimu 4121 wanahitimu katika ngazi ya cheti Shahada na
Astashahada katika mahafali ya 51 ya Chuo kikuu cha Dar es salaam
yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jiijini Dar es salaam.


Comments