SERIKALI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA VYAMA VYA KITAALUMA VYA MAAFISA UHUSIANO NA UMMA.

SERIKALI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA VYAMA VYA KITAALUMA VYA MAAFISA UHUSIANO NA UMMA.

Naibu katibu mkuu wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya habari Dk. Jim Yonazi Akifafanua jambo katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa chama cha wataalam wa mawasiliano na umma Tanzania (PRST) uliofanyika katika ukumbi wa PPF Tower jijini Dar es salaam.

Na Thadei P,Dar es salaam

Naibu katibu mkuu wizara ya mawasiliano na teknolojia ya habari Dkt Jim Yonazi amesema kuwa serikali itaendelea kushirikiana na vyama vya kitaaluma vya maafisa mahusiano na kuwataka taasisi kutoajiri watendaji wasio na taaluma ya mawasiliano ya umma kama maafisa mahusiano na Habari.

Dkt Yonaz ameyasema hayo alipokuwa akifungua mkutano mkuu wa siku mbili wa chama cha wataalamu wa mawasiliano na umma Tanzania (PRST) unaofanyika katika ukumbi wa PPF Tower jijini Dar es salaam.

Dtk Yonazi amesema kuwa ni kosa kwa mataasisi ya umma na binafsi kuajiri watumishi wasio na taaluma hiyo kama maafisa mahusiano ya umma jambo linaloharibu tasnia hiyo kwani wataalamu wa mawasiliano ya umma ndiyo watu pekee wanayeweza kuiinua suala la mahusiano ya umma nchini.

Bw. Loth Makuzi ambaye ni rais wa Chama cha Maafisa Uhusino wa Umma Tanzania, PRST amesema Mkutano wa mkuu wa chama hicho  unaofanyika Oktoba 28 na 29, 2021 jijini Dar es Salaam na umehudhuriwa na  washiriki mbalimbali kutoka Tanzania na nje ya Tanzania amesema chama hicho kitaendelea kuunganisha maafisa uhusiano hapa nchini huku akiitaja changamoto ya uwepo wa vyama viwili vya kitaaluma vinavyofanya kazi moja jambo ambalo serikali kupitia kwa katibu mkuu wizara ya mawasiliano na teknolojia ya Habari ikiahidi kulishughulikia.

Hata hivyo ameongeza kuwa katika taasisi na mashirika mbalimbali ya umma na binafsi maafisa mahusiano na umma wamekuwa hawashirikishwi katika vikao vya maamuzi na baadaye kuja kupewa tu muhtasari na maamuzi ya vikao hivyo jambo linalowapa changamoto kubwa katika utendaji kazi wao wa kila siku.

Amesema tangu kuanzishwa kwa chama hicho miaka mitatu iliyopita kimekuwa kiukiimarika kila mwaka na kuwa na mahusiano na vyama mbalimbali vya kitaaluma vya ndani na nje ya nchi ikiwemo nchi ya Kenya na Marekani.

Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa jukwaa la wahariri  nchini [TEF]Deodatus Balile amesema kama chama hicho cha kitaaluma kitadhibiti watu wasio na taaluma ya mahusiano na umma kitasaidia kuinua sekta ya habari hapa nchini huku akiwataka waandishi wa habari ambao hufanya kazi kwa karibu na maafisa mahusiano kufanya kazi zao kwa weledi.


Rais wa chama cha wataalam wa mawasiliano na umma Tanzania (PRST), Bw. Loth Makuza Akielezea historia ya chama hicho katika mkutano mkuu huo wa siku mbili uliofanyika katika ukumbi wa PPF Tower jijini Dar es salaam




Afisa mtendaji mkuu wa chama cha wataalam wa mawasiliano na umma Kenya (PRSK), Bi. Sylvia Mwichuli akizungumza wakati wa ufunguzi wa huo mkuu wa siku mbili wa chama cha wataalam wa mawasiliano na umma Tanzania (PRST), uliofanyika katika ukumbi wa PPF Tower jijini Dar es salaam




Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEC) Bw. Deodatus Balile akiongea wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa siku mbili wa chama cha wataalam wa mawasiliano na umma Tanzania (PRST), uliofanyika katika ukumbi wa PPF Tower jijini Dar es salaam.




washiriki wa mkutano mkuu wa  chama cha wataalam wa mawasiliano na umma Tanzania (PRST), uliofanyika katika ukumbi wa PPF Tower jijini Dar es salaam wakiwa kwenye picha ya pamoja.



Comments