Universal Periodic Review (UPR)yawakutanisha serikali na mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRD kujadili kwa pamoja.
Universal Periodic Review (UPR)yawakutanisha serikali na mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRD kujadili kwa pamoja.
Na Thadei Praygod
Dar es salaam
Mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRDC umekutana na wadau mbalimbali wa kutetea haki za binadamu na taasisi za kiserikali ikiwa ni siku chache kabla ya kufanyika kwa mkutano wa ujadiliwaji na upitishwaji wa za binadamu na utekelezwaji wake nchini Uswizi baadaye mwaka huu.
Akizungumza katika kikao hicho cha siku moja kuhusu Mzunguko wa tatu wa Mchakato wa Kimataifa wa Mapitio ya Hali ya Haki za Binadamu (UPR]naibu katibu mkuu wizara ya katiba na sheria Amon Mpanju amesema kuwa kikao hicho ambacho ni maandalizi ya kuelekea mkutano wa nchi Uswizi pia kitajadili mapendekezo 133 kuhusu haki za binadamu ambayo serikali imeyaridhia na utekelezaji wake katika kipindi cha miaka minne ambapo pia katika kikao hicho tume ya haki za binadamu na utawala bora ambayo ni taasisi ya serikali imeshiriki.
Mpanju ameongeza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kupigania haki za binadamu hapa nchini ambapo mapendekezo ambayo kama nchi imeyaridhia kuhusu haki za binadamu pia itajadiliwa taarifa inayohusu utekelezwaji huo na serikali itatuma wawakilishi katika mkutano unaotarajiwa kufanyika nchini Uswizi Novemba 5,2021.
Kwa upande wake mratibu wa kitaifa wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu Tanzania THRDC wakili Onesmo Olengurumwa amesema kuwa mwaka 2016 Tanzania ilipata karibia mapendekezo 290 Tanzania na ikakubali mapendekezo 133,na kuongeza kuwa mkutano huo utajadili kama nchi katika mapendekezo iliyoyakubali imetekeleza mangapi na kwa kiasi gani na baadaye watatoa mapendekezo mengine kwahiyo sasahivi tunachofanya ni kuangalia Mkutano huu katika hayo 133 Tanzania imeweza kutekeleza mangapi, pia hapo hapo tunatoa mapendekezo mengine kwa ajili ya mapitio mengine ambayo yanatarajiwa kufanyika Novemba 4, 2021
Kikao hicho cha siku moja kilichowakutanisha wadau kutoka mashirika mbalimbali ya kutetea haki za binadamu na yale ya umma kimeratibiwa na mtandao wa watetezi wa haki za binadamu THRDC kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC na shirika la Save The Children Tanzania .





Comments