FILAMU YA KLINIKI KUZINDULIWA DISEMBA 3,2021 DAR

 FILAMU YA KLINIKI KUZINDULIWA DISEMBA 3,2021 DAR 



DAR ES SALAAM

Katika kendeleza soko la filamu hapa nchini Producer Akash kwa kushirikiana na wasanii wengine wanatarajia kuzindua filamu iitwayo KLINIKI ambayo itaelezea maisha halisi wanayopitia akina mama wajawazito.

Akizungumza na wanahabari Dar es salaam juu ya ujio wa filamu hiyo mtayarishaji Akash pia filamu hiyo itaelezea umuhimu wa akina baba kuwasindikiza wenzi wao kliniki na pia itatoa picha halisi ya akina mama wajawazito furaha,na karaha wanazokumbana nazo.

Naye mmoja wa waigizaji wa Filamu hiyo aitwaye Binti Kigoma ameiomba serikali kupitia wizara ya Afya kuwasapoti katika filamu hiyokwani ina mafunzo makubwa kwa watanzania na imekuja kutokana na hali halisi ya wanawake kupitia changamoto nyingi pindi wawapo wajawazito ambapo wengi wao hawasindikizwi kliniki na waume zao.

Aidha ameongeza kuwa viongozi mbalimbali na wasanii wanatarajia kushiriki katika uzinduzi wa filamu ya KLINIKI ambayo itazinduliwa katika ukumbi wa sinema wa CITYMALL jijini Dar es salaam,Disema 3 mwaka huu ambapo watazamaji watalipa kiingilio cha shilingi 10000

Comments