JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU 8 KWA UHALIFU NA UNYANG'AYI WA KUTUMIA SILAHA

 JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU 8 KWA UHALIFU NA UNYANG'AYI WA KUTUMIA SILAHA


Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa 8 kwa tuhuma za uhalifu wa unyang’anyi kwa kutumia silaha maeneo ya Kimara.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Kamanda wa Kanda Maalumu ACP Muliro Jumanne Muliro amesema kikosi maalumu cha jesho la polisi Novemba 14 wakiwa katika majukumu yao maeneo ya kimara walijibizana kwa kutumia risasi na watuhumiwa hao na kumjeruhi jambazi mmoja na alikimbizwa hospitali kupatiwa huduma lakini alipoteza maisha.

Alisema siku ya tukio Watuhumiwa walikuwa wanajaribu kunyang’anya gari aina ya Toyota IST na Toyota Carina huku wakiwa na silaha lakini kikosi cha polisi kilifanya jitihada zake kupambana na wahalifu hao kisha kuwakamata.

Katika tukio lingine jeshi la polisi linawashikilia wahalifu wengine 6 wanaonyang’anya kwa kutumia nguvu ambapo wamekiri kufanya matukio hao Mkoani Pwani na Dar es salaam ambapo waliiba Dola 2000, saa, Laptop na Simu.

Kamanda muliro aliongeza kuwa jeshi la polisi litahakikisha wahalifu wote wanakamatwa na kufikishwa  mahakamani na jeshi limejipanga kuwadhibiti majambazi wanaotumia silaha isivyo halali

“dhumuni letu kama jeshi la polisi siyo kuuwa wahalifu ila tunajitahidi kuhakikisha kunusuru uhai wao ili kupata ushahidi ila pale wenyewe wanapojaribu kuwarushia askari wetu nasi tunajihami wakirusha moja tunarusha tatu “amesema Muliro

Amesema jeshi la polisi litaendelea kutekeleza kazi zao kwa kuzingatia sheria na kanuni halipo kwa ajili ya kumuonea mtu.

Comments