JUVICUF YABARIKI MAAMUZI YA KAMATI KUU TAIFA,YALITAKA KUMTIMUA BOBALI

 JUVICUF YABARIKI MAAMUZI YA KAMATI KUU TAIFA,YALITAKA KUMTIMUA BOBALI 


Jumuiya Vijana wa Chama cha Wananchi Cuf (JUVICUF) imelitaka baraza kuu la Taifa la chama hicho kuwafukuza uanachama mhe Hamidu Bobali na Ahmed Salim Hamis ikiwa ni siku chache tangu kupewa onyo kali na kuwa chini ya uangalizi kufatia tuhuma za kutaka kukiujumu chama hicho kujitokeza adhalani kuungana na wanachama waliofukuzwa uanachama na baraza kuu.

Akizungumza makao ya chama buguruni jijini Dar es salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa JUVICUF  Taifa Bw. Idd Mkanza amesema baraza linaunga mkono maamuzi ya baraza kuu Taifa kuwavua uanachama baadhi ya viongozi na wanachama saba wa chama akiwemo aliyekuwa mkurugenzi wa Habari Abdul Kambaya kufatia kudhibitika kuwa na mpango wa kukihujumu chama.

Alisema maamuzi yaliyofanywa na baraza kuu la chama yalifikiwa kwa mujibu wa katiba ya chama hivyo hatua ya Abdul Kambaya na Hamidu Bobali kutoka mbele ya waandishi wa habari na kuyakataa maamuzi ya kamati kuu ya chama ya kuwavua uanachama pamoja na kupewa siku 14 za kukata rufaa kama inavyoelekeza katiba ya chama wao wametishia kwenda kushitaki kwa msajili wa vyama vya siasa jambo ambalo ni kinyume katiba.

"JUVICUF taifa tunaitaka baraza kuu la taifa kumfuta uanachama mhe. Bobali ambaye kwa mujibu wa tuhuma zilizokuwa zinamkabili alipewa barua ya onyo kali na kuwa chini ya uangalizi kitendo cha kujiunga na wanachama waliovuliwa uanachama na kuendelea kumchafua Mwenyekiti Taifa Prof. Lipumba na chama kwa ujumla ni kidhibitisho tosha cha kumfuta rasmi wanachama"

Aidha jumuiya hiyo imeitaka kamati ya chama hicho kumuita na kumuhoji mwanachama mhe. Ally Faki kuwa ni kwa nini asifukuzwe uanachama kwa kushiriki katika harakati za kukidhoofisha na kukichafua chama hicho na mwenyekiti wake.


Comments