KAMPUNI YA VANILLA INTERNATIONAL LTD YAWATAKA WATANZANIA KUWEKEZA KULIMA ZAO HILO GHALI ZAIDI DUNIANI.
KAMPUNI YA VANILLA INTERNATIONAL LTD YAWATAKA WATANZANIA KUWEKEZA KULIMA ZAO HILO GHALI ZAIDI DUNIANI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Vanilla International, Simon Mnkondya akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusiana na Zao la Vanilla na jinsi linavyotajilisha watu na nchi. |
Na mwandishi wetu,Dar es salaam.
Katika kuendeleza sekta ya kilimo biashara hasa cha mazao ambayo ni ya thamani kubwa Watanzania wamehimizwa kuwekeza katika Kilimo cha Vanilla ili waweze kujikwamua kwa kupata kipato kitakachoweza kuwainua na kuinua uchumi wa nchi kwa ujumla.
Akizungumza mbele ya waandishi wa Habari Mkoani Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla International inayojishughulisha na kilimo cha Vanilla, Simon Mnkondya amesema asilimia 90 ya watanzania wengi wamejiajiri katika sekta nzima ya Kilimo hivyo kama watalima zao hilo watajiongezea maslahi makubwa katika kilimo.
Amesema fursa ya Kilimo ndio pekee ambapo wananchi wanauwezo wa kufaidika zaidi kwa kujikwamua kiuchumi na kuiwezesha nchi kuweza kwenda mbele zaidi.
"Kilimo cha Vanilla ni Kilimo ambacho kipo katika Kilimo Biashara kwani kilo moja ya zao hilo huuzwa kwa shilingi Millioni moja na pia ni miongoni mwa zao ambalo linakubalika katika mataifa ya nje. " Amesema
Amesema Kilimo cha zao la Vanilla ni miongoni wa fursa ambayo ni adhimu na inayohitajika duniani hivyo jamii ikijikita katika kilimo hicho inaweza kujikwamua kiuchumi.
Mnkondya ambaye pia ni mwamzilishi wa Taasisi hiyo alisema katika kutambua fursa zilizopo katika Kilimo cha Vanilla Taasisi hiyo iliamua kuwekeza zaidi katika zao hilo ambapo iliweza kubaini fursa mbalimbali zilizopo katika zao hilo
Amesema kampuni iliamua kuanzisha mradi katika Mkoa wa Iringa ambapo huko hutoa fursa kwa wakulima kuwekeza kwa ajili ya Kilimo hicho na badae kupata masoko kupitia kampuni hiyo hiyo.
Mndya amesema kuwa wameanzisha mradi wa kilimo cha Vanilla ambapo wanatoa fursa kwa wakulima kuwekeza na badae kupata fursa ya kuwatuzia zao hilo la vanilla na kusisitiza kuwa kampuni hiyo inanunua zao hilo kwa mkulima ambaye tayari amejisajili katika kampuni hiyo.
Mbali na hilo pia Mnkondya amesema Kampuni hiyo imefanikiwa kutoa ajira kwa vijana wakike ambao wamezalishwa watot na kutelekezwa ili waweze kujikwamua katika maisha yao kwa kupata kipato.
"Asilimia 60 ya wafanyakazi katika kampuni yetu ni wasichana ambao wametelekezwa na wanaume zao ambapo kwa mujibu wa utafiti tulioufanya tumebaini wanasichana hawa ni wavumilivu Sana. "Amesema Mnkondya
Akizungumza kuhusu kwanini mradi huo upo katika mkoa wa Njombe Mnkondya amesema Kampuni hiyo ilifanya tafiti katika baadhi ya mikoa na kubaini zao la Vanila limekuwa likiitaji ardhi ambayo inaendana na kilimo hicho.
Aidha alitoa wito kwa watanzania na wakulima kwa ujumla kwenda kutembelea mradi huo ili waweze kujifunza fursa mbalimbali na kuwekeza katika Kilimo cha Vanilla, licha ya hayo alibainisha mikoa ambayo zao la Vanilla linastawi kuwa ni Bukoba, Njome, Iringa, Mbeya na Moshi.
Comments