KANISA HALISI LA MUNGU BABA KUWAOMBEA WAJASIRIAMALI DAR

 KANISA HALISI LA MUNGU BABA KUWAOMBEA WAJASIRIAMALI DAR.



Dar  es Salaam.

Kiongozi mkuu wa kanisa Halisi la Mungu  baba jumapili hii anatarajia kukutana na kuwaombea wafanyabiashara mbalimbali wa jiji la Dar es Salaam maarufu kama 'MACHINGA' ikiwa ni mwndelezo wa ibada za kanisa hilo kuwaombea makundi mbali mbali katika jamii.

Kanisa hilo linaloongozwa na ''BABA WA UZAO'' jumapili iliyopita pia liliwaombea mama,baba lishe wa Mkoa wa Dar es Salaam ili wawe na mafanikio katika biashara zao.

Pia kiongozi huyo wa kiroho aliwasisitiza watanzania kuwa na utaratibu wa kumuombea rais wa Tanzania Mama SAMIA SULUHU HASSAN  ili aendelee  kuliletea maendeleo Taifa la Tanzania.

Tayari kanisa hilo limeshawaombea makundi mbalimbali muhimu katika jamii wakiwemo Waandishi wa Habari,Madereva wa bodaboda,Mama na baba lIshe na sasa linatarajia kuwaombea wajasiriamali wote wa Dar  es Salaam.

Aidha kanisa hilo pia linatarajia kukutana na mitume,manabii,wachungaji na wainjilist katika mkutano mkubwa unaotarajiwa kufanyika katikati ya mwezi huu katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Comments