KIMOMWE MOTORS YAMPA SHAVU NONO MKOJANI
KIMOMWE MOTORS YAMPA SHAVU NONO MKOJANI
Na Thadei P ,Dar es salaamKatika kuifanya sanaa kama kazi itakayowafanya wasanii waingize kipato Kampuni
ya uagizaji wa magari kutoka nje ya nchi Kimomwe Motors ya jijini
Dar es salaam leo imemtambulisha rasmi mchekeshaji maarufu hapa nchini
anayejulikana kama Mkojani kama balozi wa Kampuni hiyo kwa kandarasi ya mwaka mmoja.
Akizungumza
katika hafla fupi ya kumtambulisha Mkojani kama balozi wa kampuni hiyo Mkurugenzi na mwanzilishi wa Kimwomwe Motors, Bw. Selemani kimomwe amesema wameamua
kumtumia msanii huyo kama balozi wa kampuni hiyo kutokana na kufanya
kwake vizuri katika sanaa hapa nchini huku wakiamini kuwa atakuwa balozi
ambaye ataiwakilisha vyema kampuni kwa wateja wake.
"Kampuni
yetu kwa sasa ina miaka mitatu tangu tuianzishe mwaka 2018 na imekuwa
ikifanya vizuri siku baada ya siku kwani wateja wengi wameendelea
kutuamini kama sehemu yao ya uagizaji wa magari kutoka nchi za Japan,
Singapore na Uk hivyo leo tumemtambulisha mkojani kama balozi wetu
kuyaendeleza mazuri yanayopatikana ndani ya kampuni ya Kimomwe Motors"
alisema bw. Kimomwe
Akizungumzia juu ya shughuli za kampuni Meneja mkuu wa Kimomwe MOTORS Yusuph Kimomwe ameongeza kuwa kampuni hiyo
imekuwa na utaratibu mzuri wa kuhakikisha mteja atakayeagiza gari yake
kupitia Kimomwe Motors anafikishiwa gari yake ndani ya siku 45 ambapo
asilimia 50 ya thamani ya gari atailipa kabla ya gari yake kufika nchini
na kiasi kilichobaki kitalipwa baada ya gari kufika na kuongeza kuwa
endapo mteja aliyeagiza gari yake atashindwa kumalizia kiasi kilichobaki
baada ya gari yake kufikishwa nchini kampuni hiyo itamuunganisha na
taasisi ya mikopo ili kuona ni jinsi gani mteja atamalizia fedha hizo.
''ndugu waandishi sisi kama Kimomwe Motors ni miongoni mwa makampuni ambayo yanawafikishia wateja wake magari walioagiza kutoka sehemu yoyote duniani iwe Japan,Uk,Singapore au Dubai ndani ya siku 45 hivyo hatuna longolongo''alisema meneja huyo.
Hata hivyo katika hatua nyingine
kampuni hiyo imemkabidhi msanii huyo gari jipya aina ya BMW kulitumia
kwa muda kabla ya kumpatia zawadi nyingine kubwa mwezi desember mwaka
huu.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa gari hilo na kutambulishwa kama balozi wa
kampuni ya Kimomwe Motors, Abdallah Mohamed Nzunda maarufu kama Mkojani
ameishukuru kampuni hiyo kwa kumchagua kama balozi wake licha ya kuwepo
kwa wasanii wengi wanaofanya vizuri nchini na kuahidi kuwa ataitumia
fursa hiyo pia kutoa elimu kwa watanzania juu ya namna ya kuagiza gari
nje ya nchi kupitia kampuni ya Kimomwe
"Nitoe
shukrani za dhati kwa kampuni ya Kimomwe kwa kuona kipaji changu,
niwahakikishie kuwa nitafanya kazi kwa kiwango cha hali ya juu kwa
ukizingatia kampuni tayali inafanya kazi katika viwango vya kimataifa
hivyo sitawaangusha" Alisema Mkojan.




Comments