''MSIWASUJUDIE NA KUWAABUDU WACHUNGAJI MSUJUDIENI MUNGU KWA KUWAFANYA HAO VIONGOZI WA DINI''KIONGOZI MKUU KANISA HALISI LA MUNGU BABA

''MSIWASUJUDIE NA KUWAABUDU WACHUNGAJI MSUJUDIENI MUNGU KWA KUWAFANYA HAO VIONGOZI WA DINI''KIONGOZI MKUU KANISA HALISI LA MUNGU BABA



Dar es Salaam.

 Kiongozi mkuu wa kanisa halisi la Mungu Baba lililopo Tegeta,Namanga jijini Dar es salaam amewataka waumini wa dini mbali mbali kuacha kuwaabudu viongozi wa dini hizo na badala yake wamuabudu mwenyezi Mungu kwa kuwapa karama viongozi hao ya kuhubiri neno lake.

Kiongozi huyo ameyasema hayo wakati kanisa hilo lilipokutana na wachungaji,Makuhani na Manabii kutoka nchi nzima katika kongamano la neno la Mungu lililolenga kufundisha juu ya mambio mbalimbali ikiwemo juu ya kanisa halisi ni nini na juu ya kusudi la uumbaji.

Amesema kuna waumini wengi wamekuwa na tabia za kuwasujudia viongozi wao wa dini na kumsahau Mwenyezi Mungu na kuwafanya baadhi ya viongozi hao kujiona Miungu watu.

Aidha amewataka watanzania kuendelea kuiombea nchi ya Tanzania na viongozi wake ili amani iendelee kuwepo hapa nchini.

Sambamba na kuwepo kwa kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa diamond jubilee na kurushwa mubashara na kituo cha televisheni cha STAR TV pia kulishuhudiwa kufungwa kwa ndoa kati ya kuhani Hekima na kuhani Upendeleo hali iliyonogesha zaidi tukio hilo lililokuwa likifuatiliwa na maelfu ya Watanzania.

Comments