TTCL YAZINDUA KIFURUSHI KIPYA CHA BUFEE PACK KUMWEZESHA MTEJA KUCHAGUA HUDUMA KULINGANA NA SALIO LAKE
TTCL YAZINDUA KIFURUSHI KIPYA CHA BUFEE PACK KUMWEZESHA MTEJA KUCHAGUA HUDUMA KULINGANA NA SALIO LAKE
Mkurugenzi
wa Biashara wa TTCL Corporation, Bw. Vedastus Mwita akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam kwenye
uzinduzi rasmi wa huduma mpya ya kifurushi kinachojulikana kwa jina la
‘BUFEE PACK’ hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TTCL jijini Dar es
Salaam.
SHIRIKA
la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) limezinduwa huduma mpya, ya
kifurushi kinachojulikana kwa jina la ‘BUFEE PACK’. Kifurushi hicho
maalum kama zawadi kwa wateja wa mtandao wa TTCL kuelekea siku kuu za
mwisho wa mwaka kinampa mteja fursa ya kujichagulia kiwango cha muda wa
maongezi, huduma ya data na ujumbe mfupi kulingana na mahitaji yake.
Akizungumza
katika halfa ya uzinduzi wa kifurushi hicho Jijini Dar es Salaam,
Mkurugenzi wa Biashara wa kampuni hiyo, Bw. Vedastus Mwita amesema
huduma hiyo mpya ya mteja kujichagulia kifurushi kulingana na mahitaji
yake, TTCL imekuja kivingine huku lengo likiwa ni kuleta FURAHA na
TABASAMU kwa wateja.
“Safari hii tumekuja
kivingine kabisa kwa kumpa mteja fursa zaidi ya kujitengenezea kifurushi
chake mwenyewe kadri ya mahitaji yake ya Dakika, SMS na Data kwa
gharama nafuu zaidi. Mteja ataingia kwenye menyu *148*30# kisha
atachagua namba 6, mteja atapaswa kufuata maelekezo. Alisema Bw. Mwita
Alisema
TTCL kwa kumjali mteja wao zaidi, Kifurushi cha BUFEE kitakuwa hakina
UKOMO wa Muda hivyo atatumia kifurushi chake mpaka kitakapoisha kabisa
huku akipewa taarifa kulingana na matumizi.
“Hivyo,
tunapenda kuwakaribisha wateja wote kutumia fursa hii ya uwepo wa
kifurushi cha BUFEE ili waweze kufuruhia mapumziko ya mwaka wakiwa na
Data, SMS na Intaneti yenye kasi zaidi kwa gharama nafuu zaidi,”
alibainisha Bw. Mwita.
Aidha
alisema TTCL Corporation inapenda kuwashukuru wateja wake ambao
wamekuwa wadau muhimu katika kulikuza na kuliletea maendeleo Shirika na
kuahidi wataendelea kuwaletea huduma nzuri na nafuu kwa mteja ikiwa ni
kutambua mchango wao.
TTCL inatambua kuwa tupo
katika msimu wa Siku Kuu za mwisho wa mwaka hivyo tumeona sasa ni muda
muafaka wa kuwarahisishia huduma za mawasiliano hivyo kuwapa tabasamu
wateja kwa kifurushi cha kujipimia mwenyewe.
“tunambua
umuhimu wa siku kuu hizi, Shirika tumependelea kuwajali wateja wetu,
tunafahamu ni kipindi ambacho wateja na watanzania kwa ujumla wanaenda
mapumziko ya mwaka,”
Pamoja na hayo alisema
kuwa TTCL inatambua kuwa Taifa lipo katika shamrashamra za maadhimisho
ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, hivyo kifurushi hicho kitakuwa
kama faraja kubwa kwa Taifa kufikisha miaka 60 likiwa Taifa moja lenye
Amani, Ushirikinano na Umoja, huku wakifurahia matunda ya uhuru.
“Miaka
60 ya Uhuru sekta ya Mawasiliano imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwani
sasa Watanzania wanatumia huduma za simu kwa gharama nafuu na zenye
uhakika, mawasiliano yanapatikana vijijini na mijini. Kama Shirika
tumekuwa na mchango mkubwa katika kukuza matumizi ya TEHAMA na sekta ya
mawasiliano kwa ujumla.”
Mkurugenzi
wa Biashara wa TTCL Corporation, Bw. Vedastus Mwita (kushoto) pamoja na
Meneja Masoko wa TTCL Corporation, Bi. Janet Maeda (kulia) wakionesha
kwa wanahabari (hawapo pichani) wakionesha uzinduzi wa huduma mpya ya
kifurushi cha ‘BUFEE PACK’ hafla iliyofanyika Makao Makuu ya TTCL jijini
Dar es Salaam.
Comments