UMOJA WA MADEREVA BAJAJ WENYE ULEMAVU DAR WAMUOMBA RC MAKALLA KUWAONDOA WASIO WALEMAVU KATIKATI YA MJI


 

 

 DAR ES SALAAM.

Umoja  wa waendesha bajaj wenye ulemavu Dar es salaam [UWAWABADA]umemuomba mkuu wa mkoa huo,Amos Makala kutoa kauli ya kusitishwa kwa tangazo la madereva wa bajaji wasio walemavu kuingia katikati ya mji kutokana na waendesha bajaj walemavu kupitia kipindi kigumu kufuatia tangazo la kuruhusu babaj zote kuingia mjini.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam mbele ya wanahabari na mwenyekiti wa umoja huo Nyekoba Msabi na kuongeza kuwa kufuatia hatua ya wasio na ulemavu kuruhusiwa kuingiza bajaj zao katikati ya mji wao kama walemavu wameshindwa kuendana na ushindani katika biashara hiyo kwa kuchangamana na wasio na ulemavu jambo lililowapelekea kushindwa kurejesha mikopo ya bajaj walizokopeshwa na hatimaye hali kuwa ngumu.

Hata hivyo wamemuomba mkuu wa Mkoa kuliangalia upya suala hilo kwani klinawaumiza kiuchumi kutokana na kutopata kipato kinachotosheleza mahitaji yao kwani kabla ya wasio na ulemavu kuruhusiwa kuingia mjini mwezi may mwaka jana walemavu wanaoendesha bajaji walikuwa wanapata fedha zinazotosheleza mahitaji hali iliyowapelekea kukopeshwa bajaj na manispaa na wafanyabiashara wengine lakini kwa sasa wengi wao wamepokonywa bajaj hizo kufuatiwa kushindwa kufanya marejesho.

Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara walemavu Dar es salaam [UWAWADA] Juma Maleche ameipongeza hatua ya mkoa huo kuwapanga wafanyabiashara wenye ulemavu kwa ufasaha katika masoko mbalimbali huku akitoa rai kwa mkuu wa mkoa huo kuweka alama zinazoelekeza wateja maeneo wanayofanyia biashara wenye ulemavu.

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo ameutaka uongozi wa mkoa kuwadhibiti wafanyabiashara wanaorejea katika maeneo waliyokatazwa hasa nyakati za jioni.

Comments