ZAMARADI AJA NA TAMASHA LA DECEMBER TO REMEMBER

 ZAMARADI AJA NA TAMASHA LA DECEMBER TO REMEMBER

MTANGAZAJI na mtayarishaji wa filamu nchini, Zamaradi Mketema, ameweka wazi  kufanya tamasha la komedi litakalofanyika Desemba 4, mwaka huu, katika ukumbi wa Gymkana.

Akizungumza na waandishi jijini Dar es Salaam, Zamaradi amesema kuwa tamasha hilo litaongozwa na mchekeshaji kutoka nchini Uganda Anna Kansiime.

"Tamasha la komedi litafanyika Desemba 4, 2021 katika viwanja vya Gymkana na mchekeshaji maarufu kutoka nchini Uganda Anna Kansiime akisindikizwa na Mpoki, Mc Mboneke na wasanii wengi"

"Nimemchukuwa Anna Kansiime kwa kuwa anajua kuburudisha watu na kwakuwa ni tamasha letu la kwanza hatutajuta kuhuzulia,"amesema Zamaradi

Aidha ameongeza kuwa hii itakuwa ya kitofauti na matamasha mengine kwa kuwa litakuwa la kwanza na limekuwa na maandalizi ya kutosha na suprizi za kutosha.

"Kutakuwa na Komedi lakini pia michezo mbalimbali itakayowafanya watu kuburudika na kufurahi  bila kuboreka niwakaribishe watanzania wote." amesema Zamaradi

Pia amesema tamasha hill litakuwa likifanyika kila mwisho wa mwaka wa mwezi wa Disemba. 

Comments