FCC YAWAPIGA MSASA WAHARIRI WA HABARI ZA BIASHARA

 

FCC YAWAPIGA MSASA WAHARIRI WA HABARI ZA BIASHARA


Tume ya ushindani nchini Tanzania (FCC) Leo imeandaa Semina kwa wahariri wa habari za Biashara Ili kuwajengea uwezo na kuwaongezea uwelewa juu ya shughuli ambazo zinafanya  tume hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo,William Urio amesema kuwa, lengo la Semina hiyo ni kuelezea majukumu ya tume hiyo,sambamba na kuboresha shughuli zao ili walaji wa biashara wapate huduma stahiki kama wanavolipia.


Aidha amesema kuwa,  Semina hiyo imelenga  kutoa elimu stahiki kwa wahariri Ili kuhakikisha Sekta ya biashara katika nchi ya Tanzania inakua vizuri kwa kufuata kanuni na misingi inayokubalika.


Hata hivyo, amesema Kazi yao kubwa ni kukuza na kulinda kazi za Biashara pamoja na kuratibu na kuangalia shughuli hizo kwa ukaribu Ili kila mfanyabiashara anaeingia katika biashara aweze kupata matunda sahihi.


Aidha, amesema miongoni mwa mada zitakazojadiliwa katika Semina hiyo ni pamoja na majukumu ya FCC na ushindani, kumlinda mlaji pamoja na mapambano ya bidhaa bandia.


Kwa upande wake, Mjumbe wa kamati ya utendaji jukwaa la wahariri (TEF),  Nevile Meena ameiyomba Tume ya ushindani (FCC) kuwakutanisha na Taasisi zengine za umma zinazofanya kazi zinazoshabihiana ikiwemo TMDA pamoja TBS Ili waweze kuwapa elimu kuhusu mipaka ya kazi zao kwa lengo la kuandika habari vizuri.


"Tunatarajia siku moja mutusaidie kutukutanisha na Taasisi zote tatu ikiwemo FCC, TMDA na TBS kwani mnafanyakazi zinazoendana ikiwemo kupinga bidhaa bandia pamoja na kuchoma moto bidhaa feki Ili muweze kutupa elimu ya kutosha itakayotusaidia kuwaelimisha wananchi" amesema Meena.

Comments