LATRA YAKUTANA NA WADAU WA TAX MTANDAONI

 

LATRA YAKUTANA NA WADAU WA TAX MTANDAONI


 


Dar es Salaam


Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya uchukuzi) Gabriel Joseph ameitaka mamlaka ya udhibiti usafirishaji ardhini (LATRA) kusimamia maoni yaliotolewa na madereva wa tax mtandaoni Ili kutenda haki pande zote ikiwemo wamiliki wa magari, madereva pamoja na abiria.


Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam Disemba 21, mwaka huu wakati akifungua mkutano wa wadau wa Sekta ya usafirishaji ambao umelenga kupokea maoni na mapemdekezo ya nauli ambapo ameteka haki itendeke katika kufanya maamuzi.



"Naamin sana katika meza ya mariadhiano nawaomba sana mnapotoa maamuzi muangalie pande zote Ili kutenda haki, naomba muweke mizani ya haki Ili kuondoa haya malalamiko kwa wadau wote wanaoguswa na Sekta hii"amesema Joseph.


Amesema kuwa, suala la nauli ni suala ambalo linamgusa kila mtu hivyo kuna haja ya kuhakikisha kuwa kila mmoja anapatiwa fursa sawa na sehemu aliyopo.



Hata hivyo, ameitaka LATRA katika kufanya maamuzi baada ya kupokea mapemdekezo hayo ni vyema  kuweka utaratibu kanuni na sheria ili zitakazowaongoza vizuri kwa kila mmoja na eneo lake.


Aidha, amewataka madereva hao kujisajili LATRA pamoja na kurasimisha taaluma zao Ili shughuli zao ziweze kutambulika kisheria kwani kwa sasa hawatambiki kutokana na kutojusajili.



"Zaidi ni madereva kuwa rasmi na taaluma yao kuheshimiwa kwa faida ya kila mmoja itakapotokea changamoto kuwe na kanuni za kusimamia kwa kujua takwimu ya madereva wenye ajira na wasiokuwa nazo ili kujua namna ya kuweza kuwasaidia"amesema


Hata hivyo, amesema tax mtandao ni mfumo rasmi ambao bado ulikuwa haujarasimishwa ila kwa sasa wanataka kuurasimisha hivyo wajadili na kufikia maridhiano kwani wanaendelea kutekeleza kwa pamoja na anaamini kila mmoja atatekeleza makubaliano hayo.


Aidha amesema wao kama Serikali wanatambua na kuthamini mchango wanaotoa katika shughuli hizo za tax na anawashukuru wadau wote waliofikiria kuja na huduma hiyo ambapo wengi wa madereva ni vijana hivyo imesaidia kuwapatia ajira vijana hao.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji LATRA, Gillard Ngewe amesema tukio la kupokea maoni ya nauli za usafiri wa tax za mtandao unafanyika kwa mara ya kwanza kupokea maoni ndani ya siku 14 kutoa taarifa ya nauli ambazo zitakuwa zinatozwa.


Aidha amesema tax mtandao zilianza kwa mara ya kwanza mwaka 2016 baada wakiwa SUMATRA ambapo wadau waliwafuata kuomba kufahamu utaratibu wa utoaji huduma na changamoto wanazokutana nazo ikiwemo upangaji wa nauli na maeneo hivyo walishindwa kuwapatia majibu sababu walikuwa hawana mamlaka nazo.

Comments