RC DAR AITAKA TARURA KUSHIRIKIANA NA WATENDAJI SERIKALI ZA MITAA.

 RC DAR AITAKA TARURA KUSHIRIKIANA NA WATENDAJI SERIKALI ZA MITAA.




Dar es salaam

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla amewataka wakala wa barabara za mijini na vijijini TARURA kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa pindi wanapopeleka miradi ya barabara katika meneo yao

RC  Makalla ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipokuwa akifungua kikao cha kawaida cha bodi ya barabara mkoa wa Dar es salaam ambapo amesema kumekuwepo na tabia ya watendaji baadhi wa Tarura kutokuwashirikisha viongozi hao wa serikali za mitaa na vitongoji pindi wapelekapo miradi vijijini hivyo ni wakati sasa wa pande zote kushirikiana.

Aidha RC Makalla ameishukuru serikali kwa kuipatia Dar es salaam Fungu kubwa la fedha za ujenzi wa barabara kupita Tarura na kupngeza kuwa jambo hilo ni jema la litaufanya mkoa huo kuwa na barabara nzuri na za kuvutia.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam,Cate Kamba ameipongeza kauli ya Rais Samia Suluhu ya kuwa nchi lazima ikope ili kufanikisha miradi ya Maendeleo kwani nchi haiwezi kujiendesha kwa kutegemea tu mapato ya ndani.

Comments