REPOA YAWAKUTANISHA WANAFUNZI CHUO CHA DIPLOMASIA,UBALOZI WA MAREKANI KUJADILI UHUSIANO WA NCHI HIZO MBILI.

Mkurugenzi mtendaji wa REPOA Dkt  Donald Mmari akizungumza wakati wa kongamano

 

Rais mstaafu wa serikali ya awamu ya nne Dk JAKAYA KIKWETE akizungumza wakati wa kongamano la wanafunzi wa chuo cha diplomasia lililoandaliwa na taasisi ya REPOA.

RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dk.Jakaya Mrisho Kikwete amesema uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Marekani umekua wa mafanikio makubwa kutokana na Taifa linavoisaidia Tanzania


Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam wakati alipokua katika kongamano la siku moja la tathmini ya miaka 60 ya ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani ambapo amesema Taifa hilo limekua bega kwa bega na Tanzania.

Amesema kuwa, kwa miongo sita sasa Marekani imesimama na watu wa Tanzania katika kuwasaidia kufikia malengo ya maendeleo ya kitaifa kwa kuwawezesha katika nyanja mbalimbali.

Hata hivyo, amesema,  Marekani imekuwa ikisaidia maeneo ya kipaumbele yaliyobainishwa na viongozi wa Tanzania,ikiwemo Sekta ya Afya, umeme pamoja na Miundombinu ya barabara, ambapo Mataifa mengine yalikataa kuisaidia Tanzania.

"Katika uongozi wangu  nilipomuekeza Rais Obama kuhusu haja ya kuongeza upatikanaji wa umeme katika maeneo ya vijijini na kuinua tija katika kilimo kwa mara nyingine marekani ilijibu kikamilifu"amesema Rais Mstaafu Kikwete.

Kwa upande wake, Balozi  wa Marekani Nchini Tanzania Donald Wright  amesema anatarajia miaka 60 ijayo uhusiano wa Taifa la marekani na nchi ya Tanzania utaimarika zaidi kwa kuwasaidia hususani kwenye Sekta ya Afya.

"Marekani itaendelea kuwekeza katika eneo la afya ili kuhakikisha wanatokomeza janga la ukimwi ambapo hadi sasa vifo vitokavyo na ukimwi vimepungua kwa asilimia 75 na kuendelea kwekeza katika mapambano dhidi ya malaria ili baada ya miaka micache kuweza kutokomeza"amesema Donald.

Aidha amesema Serikali ya Marekani inataka kuona biashara inakuwa na Tanzania inasafirisha bidhaa kwenda Marekani ikiwemo bidhaa za viwandani.

Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Repoa Dk.Donald Mmari amesema miaka 60 imeleta manufaa makubwa kutokana na mahusiano mazuri na Marekani na Tanzania ikiwemo kuimarisha usalama wa taifa la Tanzania na uwekezaji mkubwa kama miundombinu, afya na elimu na kufungua fursa kwa Tanzania kufanya biashara Marekani

"Mahusiano kati ya Tanzania na Marekani yameimarika sana, miaka 60 imezaa matunda makubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo siasa, kiusalama pamoja na kiuchumi"amesema Dk Mmari.



Comments