MAJAJI WA MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI WAJENGEWA UWEZO KUHUSU MASWALA YA SHERIA ZA MAHAKAMA YA HIYO

 MAJAJI WA MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI WAJENGEWA UWEZO KUHUSU MASWALA YA SHERIA ZA MAHAKAMA YA HIYO


KATIKA Kuhakikisha Majaji wa Mahakama ya Africa Mashariki wanakuwa na weledi wa masuala ya sheria za nchi za Afrika Mashariki, Mahakama ya jumuia hiyo imendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo watumishi wa Mahakama hiyo.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Nestor Kayobera amesema mafunzo haya yanafanyika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa Kwa Mahakama hiyo 2001 sambamba na kuadhimishaà miaka 20 tangu kuanzishwa kwake.

"Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo Majaji wote wa Afrika wa Mahakama ya Afrika Mashariki waweze kutambua wajibu wao na kuwa na weledi sheria wa nchi wanachama wanazotoka" Alisema Jaji Kayobera.

Kwa upande Mwanasheria wa Mahakama hiyo Jaji Gerald Ndika amesema lengo mkutano huu ni kuwakutanisha majaji wa mahakama hiyo kujadilina kuhusiana na sheria zinazoweza kutumiwa na nchi wanachama katika mikataba ya Afrika Mashariki na ile ya kimataifa.

"Leo tunakutana hapa kwa lengo la kujadiliana na maswala mbalimbali kuhusiana na sheria za mahakama hiyo ambazo zinatumika katika nchi wanachama hususani katika mikataba ya ndani ya jumuia au nje ya nchi" Alisema Jaji Ndika.

Comments