MAKAMO MWENYEKITI CUF,AMSHTAKI PROFESA LIPUMBA MAHAKAMA KUU.

 MAKAMO MWENYEKITI CUF,AMSHTAKI PROFESA LIPUMBA MAHAKAMA KUU.


Dar es salaam

Makamo mwenyekiti wa CUF Taifa Mussa Haji Kombo amesema amemfungulia mashtaka mwenyekiti wa chama hicho Taifa Prof Ibrahim Lipumba kwa kile alichodai kuwa kuvunja katiba ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Makamo mwenyekiti  huyo amesema amefikia hatua hiyo baada ya kutoridhishwa mambo yanayoendelea ndani ya chama hicho ndani ya kipindi cha miaka miwili hayaleti taswira nzuri yenye kujenga taasisi hiyo zaidi ya kukidhoofisha chama.

Ameongeza kuwa baadhi ya mambo yaliyomsukuma kumfungulia kesi mahakama kuu Prof Lipumba kuwa ni pamoja na kushinikiza aliyekuwa mkurugenzi wa Habari kujiuzulu nafasi yake kwa sababu zisizoeleweka.

Mengine ni pamoja na kutohusisha viongozi wake wa karibu katika matumizi ya malimbikizo ya fedha za ruzuku ya shilingi bilioni 1.05 pamoja na kutomuhusisha makamo wake mwenyekiti wa zanzibar katika teuzi za wakurugenzi kama katiba ya chama hicho inavyohitaji.

Aidha ameongeza kuwa mashtaka mengine  aliyoyafungua mahakama kuu dhidi ya Profesa Lipumba ni suala la kusimamia kuwafukuza wanachama waandamizi na kuwapa onyo baadhi yao bila hoja na sababu za msingi na kutofuata katiba.

Hata hivyo amesema sababu hizo ndizo zilizopelekea kufungua kesi ya madai ya uvunjwaji katiba ya CUF na kuitaja kesi hiyo kuwa ni kesi namba 633/2021 Ambayo itatajwa 13/o3/2022 mbele ya  jaji Kisanya.

 

Comments