MICHUANO YA AFTER SCHOOL CLASH YAFUNGULIWA RASMI DAR ES SALAAM.



MICHUANO YA AFTER SCHOOL CLASH YAFUNGULIWA RASMI DAR ES SALAAM.







Dar es salaam

Taasisi ya ukuzaji michezo Tanzania Nass Sports Solutions [NSS]leo imezindua michuano ya mpira wa miguu ijulikanayo kama After School Clash.

Akizungumza katika ufunguzi wa michuano hiyo,mkurugenzi wa taasisi hiyo Nassoro Mungaya amesema michuano hiyo itakuwa ni maalum kwa wahitimu wa kidato cha nne na sita ambao wamehitimu masomo yao na kusubiri matokeo.

Amesema lengo la michuano hiyo ni kuendelea kukuza michezo hapa nchini ndani na nje ya shule na wanatarajia kuipeleka pia michuano hiyo nchi nzima.

Hata hivyo mkurugenzi huyo ameongeza kuwa kwa sasa michuano ya After School Clash kwa sasa imeanza na shule nane za mkoa wa Dar es salaam na baadaye yataendelea nchi nzima huku akiwataka wadau kujitokeza kudhamini michuano hiyo.

Shule zinazoshiriki michuano hiyo kwa sasa ni pamoja na Alpha sekondari,Ahmes sec,Crown sec,Marian Boys sec,Rosmin sec,ST joseph boys sec,Heritage secondary pamoja na shule ya wavulana ya Abbey secondari


Comments