MKUTANO MKUU MAALUM ACT WAZALENDO WAFANYIKA KWA KISHINDO DAR
MKUTANO MKUU MAALUM ACT WAZALENDO WAFANYIKA KWA KISHINDO DAR
Na Mwandishi wetu
Dar es salaam
Chama cha ACT WAZALENDO kinaendelea na mkutano wake mkuu maalum kumchagua mwenyekiti wa chama hicho katika ukumbi wa mlimani city,Dar es salaam.
Miongoni mwa wageni mashuhuri na vyama rafiki vilivyoalikwa katika mkutano huo mkuu maalum ni pamoja na Rais wa chama Cha CCC cha nchini Zimbabwe Nelson Chamisa ambaye pia alishiriki katika hafla ya chama hicho kuzindua programe yake mpya inayojulikana kama 'ACT kiganjani ambayo itawawezesha wanachama wa chama hicho kujisajili na kupata kadi ya chama kidigitali.
Mbali na hayo pia chama hicho kimeendelea kujinasibu kuwa miongoni mwa vyama vinavyoendeshwa kisasa zaidi kwa kuwa na mifumo bora ya kidigitali pamoja na kujiendesha kidemokrasia zaidi ambapo pia kimefanya mdahalo kwa wagombea wa nafasi ya uennyekiti.
Zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali za mkutano huo maalum mkuu wa ACT.
Wanachama wa chama cha ACT wazalendo |
picha za wagombea wa nafasi ya mwenyekiti wa chama cha ACT Taifa |
wajumbe wakiendelea na zoezi la uchaguzi katika ukumbi wa mlimani city |
Kiongozi mkuu nwa chama cha ACT WAZALENDO Zitto Kabwe akipokea kadi yake ya uanachama wa chama hicho kutoka kwa Rais wa chama cha CCC Nelson Chamisa |
Rais wa chama cha CCC cha nchini Zimbabwe Nelson Chamisa akizungumza katika mkutano mkuu wa chama cha ACT wazalendo ambapo amekipongeza chama hicho kinavyoendesha chaguzi zake za ndani |
Comments