MRITHI KITI CHA MAALIF SEIF ACT WAZALENDO KUJULIKANA JANUARY 29
MRITHI KITI CHA MAALIF SEIF ACT WAZALENDO KUJULIKANA JANUARY 29
Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe MDC Nelson Chamisa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano Mkuu Maalumu wa chama cha ACT Wazalendo ambao unatarajiwa kufanyika Januari 29 Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za chama hicho zilizopo Kijitonyama,Dar es salaam katibu mkuu wa ACT Wazalendo,Ado Shaibu amesema mkutano huo utahusisha pia uchaguzi wa baadhi ya viongozi wakuu wa chama hicho pamoja na uzinduzi wa progrm ya kimtandao ya ‘ACT kiganjani’.
Aidha amesema katika mkutano huo wanatarajia kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi ya mwenyekiti wa chama hicho ambayo ilikuwa ikishikiliwa na hayati Maalim Seif Sharif Hamad pamoja na makamo mwenyekiti wa chama pamoja na mjumbe mmoja wa Kamati kuu Ya chaama hicho.
Aidha kuhusiana na program ya ACT kiganjani amesema imelenga kusaidia katika kuiwajibisha serikali kutokana na uchache wa wabunge wa upinzania bungeni hivyo wataitumia kama njia ya kufichua changamoto zinazowakabili wananchi hususan vijijini ambapo wanakosa wa kuwasemea.
Hata hivyo katika mkutano huo vyama vyote vya siasa hapa nchini vimealikwa katika mkutano huo pamoja na baaadhi ya vyama vya siasa nje ya nchi ikiwemo NDC kutoka zimbabwe,ODM kutoka Kenya,NUP cha Uganda,UPND Zambia,UPM Malawi pamoja na chama cha UNC cha jamhuri ya kidemokrasia ya Congo DRC.
Mkutano huo mkuu maalum unatarajiwa kutanguliwa na mikutano mingine miwili ya tarehe 27 na 28 january 2022 na utahusisha wasanii mbalimbali na vyombo vya habari huku akiwataka wanachama wa ACT wazalendo kuendelea kuwa na imani na chama chao.
Comments