NAIBU WAZIRI WIZARA YA ARHI ARIDHISHWA NA MAENDELEO ,MRADI UJENZI NHC MOROCCO SQUARE
NAIBU WAZIRI WIZARA YA ARHI ARIDHISHWA NA MAENDELEO ,MRADI UJENZI NHC MOROCCO SQUARE
SERIKALI Imeridhishwa na mwenendo wa mradi wa ujenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) wa Morocco Square ambao umefikia asilimia 93.
Akizungumza baada ya kufanya ziara ya kutembelea mradi huo kuona maendeleo yake Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amesema ameridhishwa na namna mradi huo ambao umefikia aslimia 93.
“Kwa mujibu wa maelezo niliyopatiwa Mradi huu umefikia asilimia 93, unakaribia kwisha. Kilichokuwa kimeukwamisha ni upatikanaji wa fedha, hivyo kilichobaki nikutafuta hizo fedha ili kukamilisha mradi na tayali tumeshapewa ruhusa ya kuzitafuta,” alisema Kikwete.
Alisema napenda kuipongeza NHC kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kusimamia vizuri miradi yao inayoendelea katika maeneo mbalimbali nchini niwahidi kushirikiana na nyie kuhakikisha changamoto zote zinatatuliwa haraka ili mradi huo ikamilike.
“Nimeridhishwa na mradi huu tuendelee kutafuta fedha ili mradi ukamilike kwa wakati, ofisi yangu hitahakikisha natoa ushirikiano utakaohitajika,” Alisema Kikwete.
Aidha alisema ameitembelea NHC ili kutambua na kujifunza juu ya shirika hilo na kutambua changamoto linazokabiliana nazo na kuzitafutia ufumbuzi.
Nae Mkurugenzi wa NHC, Bw. Maulidi Manyani alisema mradi huo mpaka kukamilika kwake unagharimu zaidi ya bilioni 137 ambapo hadi sasa umeshagharimu jumla ya shilingi bilioni 112.4.
Alisema shilingi bilioni 25.7 zinahitajika kukamilisha sehemu iliyobaki katika mradi huu mpaka ukamilike tayali shirika limeshaandaa mkakati wa kutafuta fedha hizo.
“Shirika tayali limeshaandaa mkakati wa kutafuta fedha hizo na tumeshapatiwa ridhaa ya kuzitafuta hivyo basi nikuhakikishie mhe waziri mradi huu utakamilika kama ilivyopamgwa,” Alisema Banyani
Comments