THRDC YATEMBELEWA NA SHIRIKA MWANACHAMA WA MTANDAO TANZANIA YOUTH BEHAVIORAL CHANGE ORGANIZATION (TAYOBECO)

 THRDC YATEMBELEWA NA SHIRIKA MWANACHAMA WA MTANDAO TANZANIA YOUTH BEHAVIORAL CHANGE ORGANIZATION (TAYOBECO)





***************

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), leo umetembelewa na shirika mwanachama wa mtandao linalojishughulisha na utetezi wa Haki za vijana na makundi maalum TAYOBECO.

Katika kikao hicho mkurugenzi wa TAYOBECO,Bi. Shida Kabulunge akiambatana na maafisa wengine wanne (4) wa TAYOBECO akiwemo Mwakilishi wa vijana NacoNGO Bw. Rogers Fungo kwa pamoja  wamepata fursa ya kukutana na kufanya mazungumzo na Mratibu kitaifa  wa mtandao, Bw. Onesmo Olengurumwa pamoja na Afisa dawati la wanachama Bi. Lisa Kagaruki.

TAYOBECO wamejadiliana juu ya namna bora ya kuimarisha mashirikiano baina yake na THRDC kama wanachama wa mtandao, na namna wanaweza kutumia fursa zilizopo katika mtandao kwa lengo la kuimarisha shughuli za utetezi wa haki za vijana na makundi maalum kwa mwaka wa 2022.

Moja ya eneo kubwa ambalo TAYOBECO imehitaji kushirikiana na Mtandao ni katika upatikanaji msaada wa kisheria, elimu ya usalama wa kidigitali pamoja na namna ya kupata fursa za kukutana na wadau watakaiwezesha taasisi katika upatikanaji wa rasilimali fedha.

Mazungumzo hayo ni mwendelezo wa mazungumzo yaliyofanyika mwaka jana (2021) baina ya mtandao na taasisi hii ya TAYOBECO uliolenga kuendeleza mashirikiano baina ya taasisi hizi mbili, lakini pia THRDC imekuwa ikiwaunganisha wanachama wake na fursa mbali mbali zinazopatikana kutoka kwa wadau kwa lengo la kuimarisha na kukuza shughuli za utetezi wa haki za binadamu nchini.



*Imetolewa na Afisa Habari, THRDC*

*21 Januari, 2022*


Comments