Wahitimu Wa NCT Waaswa Kuangalia Masoko Ya Utalii Wa Ndani

 


NAIBU waziri wa Maliasili na Utalii, Mery Masanja amewaasa wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT)wakaangalia masoko ya utalii wa ndani ili kuwashawishi wananchi kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini na kuweza kujifunza vivutio tulivyonavyo.

Amayasema hayo leo Januari 21, 2022 wakati wa Mahafali ya 19 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaama, amesema baada ya mahafali hayo wakafanye kwa vitendo waliyojifunza Darasani.

"Niwaombe mkatumie vizuri ujuzi mlioupata kwa kutekeleza majukumu yenu, kwa uadilifu na weledi ili kukuza sekta yetu ya Utalii pamoja na kujenga nchi yetu kwa kuwa mabalozi wazuri wa chuo chetu cha Taifa cha utalii." Amesema Mery.

Amesema kuwa kutokana na ushawishi wa  Rais samia serikali imepokea fedha kutoka shirika la fedha duniani (IMF) kwaajili ya kukabiliana na athari zitokanazo na janga la Uviko 19.

Ameelezea kuwa sehemu ya fedha hizo zimeelekezwa wizara ya maliasili na utalii kwaajili ya kutumika kununua vitendea kazi, kuboresha miundombinu ya utalii nchini  pamoja na maeneo ya Vivutio vya utalii.

Pia amesema kuna fedha zimetengwa kwajili ya utangazaji na kutoa mafunzo kwa watoa huduma za utalii nchini.

Licha ya hayo amewaomba wahitimu hao kuunga mkono juhudi za Rais Samia katika kuboresha huduma katika tasnia ya Utalii nchini.

Mery amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassani kwa kuwa mdau namba moja wa Utalii nchini kwa kuonesha njia na namna ambavyo tunapaswa kuonesha utalii wetu kwa dunia.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utalii wizara Maliasili na Utalii, Philip chitaunga amesema kuwa Utekelezaji wa sera ya Taifa ya utalii  ya mwaka 1999 ndio unafanya uwepo wa chuo hicho na kuendelea na majukumu yake ambayo leo wahitimu 541 wanatunukiwa vyeti vyao.

Katika Mahafali hayo ya 19 chuo cha Taifa cha Utalii, Wahitimu Waliotunikiwa Vyeti vyao ni kutoka kozi tofauti tofauti ambazo ni Stashahada ya Ukarimu wahitimu 104, Astashahada ya Ukarimu ni 5 Astashahada ya upishi 66, Astashahada ya huduma za Chakula na Vinywaji 17, Astashahada ya utunzaji wa Vyumba na Ufuaji 6, Astashahada uratibu wa Matukio 33, Astashahada ya uokoaji 15, Astashahada ya Usafirisha na Utalii 105, Astashahada ya usafirishaji watalii 92, na  Astashahada ya Uongozaji wa watalii. Wakiwa na Jumla ya 541.
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Mery Masanja akizungumza wakati wa Mahafali ya 19 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaama leo Januari 21, 2022
Mkurugenzi wa Utalii wizara Maliasili na Utalii, Philip chitaunga akizungumza wakati wa Mahafali ya 19 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaama leo Januari 21, 2022
Ofisa Mtendaji mkuu NCT Dkt. Shogo Mlozi akizungumza wakati wa Mahafali ya 19 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaama leo Januari 21, 2022.
Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Taifa wakiwa katika Mahafali ya 19 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaama leo Januari 21, 2022
Wahitimu wa Chuo cha Taia cha Utalii (NCT)wakiurahia jambo katika Mahafali ya 19 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaama leo Januari 21, 2022.

Baadhi ya wacheza ngoma ya Mwanaliombe 

Baadhi ya wahitimu wakionesha mavazi ya Kiafrika wakati wa Mahafali ya 19 ya chuo hicho yaliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaama leo Januari 21, 2022.

Comments