INDIA NA TANZANIA ZAZIDI KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA MBALIMBALI NCHINI.
INDIA NA TANZANIA ZAZIDI KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA MBALIMBALI NCHINI.
Dar es salaam
Ushirikiano baina ya nchi na nchi limekuwa jambo muhimu katika kuongeza chachu ya maendeleo ya kiuchumi,kisiasa,kidiplomasi baina ya nchi hizo husika.
Balozi wa India Nchini Tanzania Binaya Pradhan amesema Tanzania na India mahusiano yao yanazidi kukua kwa kushirikiana katika sekta mbalimbali za uchumi na uwekezaji.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam Balozi Pradhan amesema licha ya changamoto za ugonjwa wa Covid 19 India kwa sasa hali ya kiuchumi imeimarika kutokana na wananchi wake kupata chanjo na kupunguza maambukizi ya virusi hivyo.
Aidha amesema ushirikiano kati ya Tanzania na India unazidi kuimarika katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Ulinzi hususani katika usalama wa bahari ya hindi na kukabiliana na vitendo vya kigaidi.
Aidha amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zinaingiza bidhaa nyingi nchini India ikiwemo madini na parachichi ambazo kwa sasa wamezipunguza toza ili kuzidi kuimarisha biashara baina ya Tanzania na India.
Hatahivyo amesema makampuni mengine nchini India yameonyesha nia ya kuja kuwekeza nchini Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo viwanda vya sukari na dawa, sekta ya elimu, mafuta, gesi, chakula na Afya.
Comments