Machinga na bodaboda Dar wafunika,Mapokezi Ya Rais Samia Akitokea Ubelgiji

 

Machinga na bodaboda Dar wafunika,Mapokezi Ya Rais Samia Akitokea Ubelgiji 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Philip Isdor Mpango pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Februari, 2022

.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam waliofika kumpokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Februari, 2022 mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi katika nchi ya Ufaransa na Ubelgiji.

Sehemu ya Wananchi wakishangilia mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Februari, 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais Mhe. Philip Isdor Mpango pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Februari, 2022. 
 
  
 
  



Umoja wa machinga jijini Dar es salaam pamoja na madereva wa bodaboda jijini humo wamefika kwa wingi katika mapokezi ya Rais Samia Suluhu na kupendezesha shamrashamra za mapokezi ya kiongozi huyo mkuu wa nchi,


Katika mapokezi hayo machinga hao waliongozwa na katibu wa wamachinga ambapo msafara wa kumpokea Rais Samia ulitokea katika viwanja vya sabasaba.


Comments