MKUCHU CUP 2021/22 YATAMATISHWA DSM HUKU TANGA BOYS WAKIIBUKA MABINGWA WA MICHUANO HIYO.

MKUCHU CUP 2021/22 YATAMATISHWA DSM HUKU TANGA BOYS WAKIIBUKA MABINGWA WA MICHUANO HIYO.


Meya wa manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akizungumza mara baada ya kutamatishwa kwa fainali ya Mkuchu CUP 2021/22 Katika viwanja vya Machava,Kunduchi jijini Dar es salaam 

Meya wa manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akikabidhi kombe la ushindi na bodaboda kwa nahodha wa timu ya Tanga Boys  baada ya kutamatishwa kwa fainali ya Mkuchu CUP 2021/22 Katika viwanja vya Machava,Kunduchi jijini Dar es salaam ambapo timu hiyo iliibuka mshindi


Mwandaaji wa mashindano hayo ambaye pia ni Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kilongawima Emmanuel Mkuchu  akizungumza mara baada ya kutamatishwa kwa fainali ya Mkuchu CUP 2021/22 Katika viwanja vya Machava,Kunduchi jijini Dar es salaam 




Timu za Tanga BOYS na Nondo FC zikiwa uwanjani.


sehemu ya mashabiki waliohudhuria fainali ya michuano ya Mkuchu Cup 2021/22 wakiutazama kwa makini mchezo huo katika uwanja wa Machava ,Kunduchi


Na Thadei PrayGod

 Dar es salaam.

Fainali ya Michuano  ya mpira wa miguu ya MKUCHU CUP 2021/22 imemalizika rasmi huku timu ya Tanga Boys ya Kunduchi ikiibuka mshindi wa michuano hiyo kwa kuichapa timu ya Nondo FC yenye maskani yake Msisiri,Mwananyamala kwa goli 1 kwa 0.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mtanange huo meya wa manispaa ya Kinondoni,Songoro Mnyonge ameipongeza michuano hiyo kwa kusema kuwa imewaunganisha vijana si tu wa kata ya kunduchi bali wilaya nzima ya Kinondoni na Mkoa wa Dar es salaam kiujumla kwani imezikutanisha timu mbalimbali za ndani na nje ya wilaya hiyo.

Songoro amesema kuwa michuano hiyo ya Mkuchu Cup imeonyesha ni jinsi gani vijana wanaweza kuungana kwa pamoja katika sekta ya michezo na kuunga mkono jitihada za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kuiboresha sekta ya michezo hapa nchini.

''hakika nawapongeza sana waandaaji wa michuano hii  ya Mkuchu Cup kupitia ndugu yangu Emmanuel Mkuchu ambayo imeshatazamwa na karibia watu elfu 20 tangu Kuanza kwake,na niipongeze pia kampuni ya Meridian Bet na taasisi ya bega kwa bega na mama na hili nataka liwe mfano kwa kata na mitaa mingine kuandaa michuano ya namna hii ambayo huleta chachu ya michezo na ari kwa vijana''alisema Meya Songoro.

Kwa upande wake mwandaaji wa michuano hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali ya mtaaa wa Kilongawima,Emmanuel Mkuchu amesema aliamua kuandaa michuano hiyo si tu kuwanganisha vijana kupitia michezo pekee bali kuwahamasisha wananachi kushiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika mwezi Agosti mwaka huu.

''ndugu zangu waaandishi wa Habari mimi kama kijana na kiongozi wa serikali za mitaa nilihamasika na nikaona si vibaya kuanzisha michuano hii nikishirikiana na wadhamini wetu Meridian Bet na Bega kwa bega na mama na naamini katika michuano hii tumewahamasisha vya kutosha wanannchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa ya watu na makazi 2022 na nawaomba siku hiyo washiriki kikamilifu ili kundeleza juhudi za serikali katika kuletea Taifa letu Maendeleo''alisema Mkuchu.

Mkuchu ameendelea kusema kuwa michuano hiyo imehusisha timu 20 za ndani na nje ya Kunduchi ambapo mshindi wa kwanza  ambaye ni timu ya Tanga Boys imejishindia pikipiki yenye thamani ya zaidi ya milioni 2.6 na kombe la ushindi huku mshindi wa pili ambaye ni timu ya Nondo FC ikijinyakulia kitita cha shilingi milioni moja taslim.

Naye mwenyekiti wa taasisi ya bega kwa bega na mama,Mohamed Hassan amesema wameamua kuungana na waandaaji wa fainali ya Mkuchu Cup ili kuungana na Rais Samia katika kuinua sekta ya Michezo hapa nchini hivyo wao kama taasisi wataendelea kuwaunga mkono watanzania wote wenye mapenzi mema na Taifa.

Hata hivyo Kampuni iliyodhamini fainali hizo ya Meridian Bet kupitia Twaha Ibrahim wa kitengo cha masoko cha kampuni hiyo amesema michezo imekuwa chachu ya maendeleo kwa vijana ndiyo maana kampuni hiyo ikaamua kuidhamini Mkuchu Cup huku mkaazi wa kata ya Kunduchi Bi Twilomba Jane Balama akitoa Rai kwa Rais Samia kuendelea kuishika mkono sekta ya michezo sambamba na kumpongeza mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Kilongawima kwa utthubutu wake kupitia fainali hizo.

Comments