WAJUMBE WAPYA BODI YA TAASISI YA MWALIMU NYERERE FOUNDATION WATAMBULISHWA
WAJUMBE WAPYA BODI YA TAASISI YA MWALIMU NYERERE FOUNDATION WATAMBULISHWA
WAJUMBE WAPYA BODI YA TAASISI YA MWALIMU NYERERE FOUNDATION WATAMBULISHWA
Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNF) imewatambulisha wajumbe wapya nane wa bodi ya Taasisi hiyo ambao wanafanya kuwa na idadi ya wajumbe 10, huku ikimteua Joseph Butiku kuwa Mwenyekiti wa Taasisi.
Aidha, wajumbe hao, ni pamoja na Balozi Amina Salum Ali,Neema Nyerere Drago,Geofrey Israel Kirenga, Kathryn Ngenda Kigaraba,John Joel Kyaruzi,Balozi Celestine Christopher Liundi,Profesa Penina Oniviel Mlama, Profesa Martha Ambrose Suley Qorro,huku wajumbe wa zamani akiwa ni Joseph Butiku na Profesa Tarsis Bazana Kabwegyere.
Akizungumza mara baada ya kutambulisha wajumbe hao Mwenyekiti mpya wa MNF Joseph Butiku amesema kwamba tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo miaka 26 iliyopita imekua ikisimamia Serikali katika masuala ya Amani,Umoja na Maendeleo ya Watu.
Aidha amesema kwamba Malimu Julius Kambarage Nyerere alianzisha Taasisi hiyo mara baada ya kustaafu uongozi ikiwa lengo ni kusimamia misingi ya Utu,Umoja na Kudumisha Amani pamoja nakuhimiza wananchi katika kujiletea maendeleo.
Amesema Taasisi hiyo licha yakukumbwa na changamoto mbalimbali imekua na heshima kubwa kwa Taifa nakwambia uongozi uliopo utaendelea kusimamia misingi iliyoasisiwa na baba wa Taifa pindi akianzisha Taasisi hiyo kwa ajili yukuwaletea maendeleo Watanzania.
" Taasisi yetu tumekua tukijikita kuwafikia wananchi nakuwahimiza wawe na Umoja na mshikamano,pasipo na Umoja hakuna maendeleo,hivyo tunawaelimisha wawe na Umoja na kufanya kazi za kuwaletea maendeleo" amesema Butiku.
Kwa upande wake aliekua Kaimu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba amesema kwamba tangu kuanzishwa kwa Taasisi hiyo imepata mafanikio mbalimbali ikiwemo kupata jengo linalotumika kama kitega uchumi na ofisi nakwamba watapata fedha za kuendesha Taasisi.
" Tulianza kutafuta kitega uchumi na tukapata kiwanja Mtaa wa Sokoinne karibu na ukumbi wa Karemjee,lakini wakati tulipotaka kuanza ujenzi Serikali ikasema hairuhusiwi kujenga jengo la zaidi ya ghorofa sita karibu na Ikulu hivyo ikatupatia kiwanja kingine Mtaa wa jiji ndo tumejenga jengo " amesema Jaji Warioba
Nakuongeza ,licha yakua na jengo hili bado hatujapata fedha za kutosha , tunaomba msaada kwa Serikali na wadau mbalimbali, manake hatuna fedha kutokana na kukosa wapangaji wa uhakika baada ya Serikali kuhamia Dodoma pamoja na mripuko wa ugonjwa wa UVIKO 19 ambao ulitokea miezi michache baada ya jengo hilo kufunguliwa.



Comments