MWENDOKASI 'FULL KIYOYOZI' KUANZA KUTUMIKA DAR ,DART YAJIVUNIA MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA MADARAKANI.

MWENDOKASI 'FULL KIYOYOZI' KUINGIA NCHINI,DART YAJIVUNIA MWAKA MMOJA WA RAIS SAMIA MADARAKANI.


Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede akizungumza na waandishi wa habari wakati akieleza mafanikio ya DART ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani


NA THADEI PRAYGOD DAR ES SALAAM

  • 'Ni full Kiyoyozi' hiyo ndiyo kauli ambayo unaweza kusema mara baada ya wakala wa mabasi yaendayo kasi kutangaza kuleta mabasi ya mwendokasi ambayo yatakuwa yana viyoyozi 'AC' ili kuondokana na adha ya joto ambalo abiria hukumbana nalo katika usafiri wa umma jijini hapa,na kwa kuwa watoto wa mjini husema Dar Joto basi ujio wa mabasi haya wala hautawalazimu abiria hao kutoa leso kujipepea kwani utakuwa ni mwendo wa full kiyoyozi.
Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Mhede wakati akieleza mafanikio ya wakala huo mwaka mmoja baada ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia SULUHU Hassan kuingia madarakani ambapo amesema hatua hiyo inafuatia malalamiko ya abiria wakilalamikia mabasi hayo kukosa viyoyozi jambo linalowapa kero hivyo ujio wa mabasi 95 yenye viyoyozi ambayo yanatarajiwa kuingia nchini mwishoni mwa mwaka huu yatapunguza adha hiyo.

''sisi kama wakala katika kipindi hiki pia kabla mwaka huu kumalizika tutaingiza mabasi 95 katika lot hii ya kwanza ya barabara ya morogoro kuanzia kimara hadi kivukoni na Gerezani hivyo kama abiria atakuwa amejipulizia pafyumu yake na kuhofia kuwa akipanda mwendokasi mpaka afike mwisho harufu ya manukato itakuwa imeisha hilo hapana sasa watapata raha kwani mabasi hayo yakuwa na viyoyozi kuanzia mwanzo hadi mwisho wa safari''alisema Dkt Mhede.

Aidha Dkt Mhede ameeleza maeneo ambayo Wakala huo unajivunia kufanya vizuri kwa kipindi cha mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani,kuwa ni pamoja na maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya usafiri katika mwaka mmoja wa Serikali ya awamu ya Sita wamefanikiwa kukamilisha ujenzi wa karakana ya ubungo iliyogharimu kiasi cha bilioni 15 yenye uwezo wa kuhifadhi mabasi 75 hadi 100  hivyo kuwa msaada wa karakana ya Jangwani.

Dkt Mhede amesema ujenzi wa miundombinu na barabara za mabasi yaendayo haraka uko katika awamu sita ambapo awamu ya kwanza ilishakamilika na inaendelea kutoa huduma ya usafiri na katika ujenzi wa miundombinu ya awamu ya pili ambao unajumuisha barabara ya Kilwa, tawi la barabara ya Kawawa yenye jumla ya kilometa 20.3. ambao nao unaendelea na ujenzi 

“Ujenzi kwa awamu ya pili unafanywa kwa mafungu mawili, fungu la kwanza ni ujenzi wa barabara na vituo vya mabasi katikati ya barabara kuu ya Kilwa, fungu la pili ni ujenzi wa majengo yaani vituo mlisho Karakana na vituo vikuu “. Amesema Dkt.Muhede.

Ameeleza kuwa hatua iliyofikia kwenye ujenzi wa awamu ya pili fungu la kwanza ni asilimia 50.07% hadi kufikia machi 2022 ikilinganishwa na asilimia 11.82% machi 2021 huku akiahidi mradi huo kumalizika na kuanza kutoa huduma mpaka kufikia mwezi machi 2023 hivyo hayo ni mafanikio makubwa tangu Rais Samia aingie madarakani.

Hata hivyo ameongeza kuwa Dart wameongeza mradi mpya ujulikanao kama E-BAJAJ ambao utawawezesha abiria wanaoshuka katika vituo kutumia usafiri wa bajaji kwenda katika maeneo mengine  zitakazotumia nishati jadilifu ikiwa na mikakati ya wakala huo katika kupunguza hewa ya ukaa







Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede akizungumza na waandishi wa habari wakati akieleza mafanikio ya DART ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani


Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Usimamizi wa miundombinu DART, Dkt.Philemon Mzee akizungumza na Waandishi wa Habari wakati DART ikieleza mafanikio ya DART ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi yaendayo kwa haraka (DART), Dkt.Edwin Muhede akiwa pamoja na watumishiwa DART wakitembelea daraja la juu la Mabasi yaendayo haraka katika makutano ya barabara Uhasibu na Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam wakati akifanya ziara na waandishi wa habari kuangalia miundombinu ya barabara ya Mabasi yaendayo haraka awamu ya pili.

Daraja la juu la Mabasi yaendayo haraka katika makutano ya barabara Uhasibu na Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam ujenzi ukiendelea






Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Usafiri DART Mhandisi Fanuel Kalugendo akizungumza na Waandishi wa Habari wakati DART ikieleza mafanikio ya DART ndani ya mwaka mmoja wa Serikali ya Awamu ya Sita Madarakani.


Comments