PUMA ENERGY TANZANIA YATOA PONGEZI KWA MAWAKALA WA KAMPUNI HIYO

 

PUMA ENERGY TANZANIA YATOA PONGEZI KWA MAWAKALA WA KAMPUNI HIYO.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Puma Energy Tanzania Dkt. Selemani Majige akimkabidhi zawadi mshindi kwenye masuala ya utoaji huduma kwenye jamii katika vituo vya mafuta  vya kampuni ya Puma Energy Tanzania kwenye hafla ya utoaji wa Zawadi kwa mawakala (Dealers) wa vituo vya mafuta vya Puma Energy nchini iliyofanyika leo tarehe 24/03/2022 Jijini Dar es Salaam.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Puma Energy Tanzania Dkt. Selemani Majige akimkabidhi zawadi mshindi kwenye masuala ya utoaji huduma kwenye jamii katika vituo vya mafuta  vya kampuni ya Puma Energy Tanzania kwenye hafla ya utoaji wa Zawadi kwa mawakala (Dealers) wa vituo vya mafuta vya Puma Energy nchini iliyofanyika leo tarehe 24/03/2022 Jijini Dar es Salaam.



DAR ES SALAAM

Waendeshaji wa Vituo vya Mafuta vya Kampuni ya Puma Energy Tanzania wamepongezwa kwa kuhakikisha mafuta yanakuwepo muda wote kwenye vituo vilivyopo nchini.

Ameyasema hayo leo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Puma Energy Tanzania Dkt. Selemani Majige katika hafla ya utoaji wa Zawadi kwa mawakala (Dealers) wa vituo vya mafuta vya Puma Energy nchini iliyofanyika leo tarehe 24/03/2022 Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuna umuhimu wa waendesha vituo hivyo kuendelea kuhakikisha mafuta ya kampuni hiyo yanakuwa bora katika vituo vyote nchini ili kuweza kulinda kukuza jina la kampuni hiyo.

Amepongeza Menejimenti ya Puma Energy Tanzania kwa kuhakikisha yale malengo ambayo walijiwekea kwamba wanafikia au wanaongeza vituo vya mafuta nchini hatimae malengo hayo yanaonekana kutimia.

“Mwaka 2018 wakati naanza kuwa mwenyekiti wa Bodi tulikuwa na vituo 52, lakini leo tunasema tumefikia vituo 80, hivyo napenda kuwapongeza wafanyakazi wa Puma Energy Tanzania pamoja na Bodi ya Puma kwa kazi na kutoa maelekezo kuhakikisha kwamba tunafikia malengo ambayo tumekubaliana”. Amesema

Hata hivyo amesema wanaendelea kushughulikia suala la kuwepo kwa vituo vidogovidogo vya mafuta vijijini ili kuongeza upatikanaji wa mafuta nchini.

“Tunayo furaha kujumuika na mawakala wote wa Puma Energy kwa mwaka 2022. Lengo sio tu kufurahi mafanikio yetu, lakini kutambua juhudi kubwa iliyowekwa kwenye maeneo mbali mbali”. Amesema

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Puma Energy Tanzania Bw. Dominic Dhanah amesema wameendelea kuongeza ubunifu na kuingiza bidhaa mpya Sokoni, mwaka 2021 waliingiza bidhaa mpya za Puma Lubricants, ambapo zimepokelewa vizuri Sokoni.

“Tunaomba muendelee kupigia kampeni vilainishi hivi vya Puma ili vikubalike zaidi sokoni na mtupe mrejesho wa namna tunavo weza kuboresha zaidi bidhaa hizi”. Amesema Bw.Dhanah.

Bw.Dhanah amesema mwaka huu 2022 walitegemea kuzindua bidhaa za gesi ya majumbani maarufu kama LPG hivyo Mawakala watakuwa wadau wakubwa na wanufaika wakubwa wa bidhaa hiyo,  itapokelewa vizuri sokoni na kutengeneza thamani zaidi katika biashara zenu na katika kampuni yetu ye Puma Energy kwa ujumla.

Comments